Pages

MJUMITA: TUCHAGUE VIONGOZI WATAKAO TETEA USIMAMIZI ENDELEVU WA MISITU

Mtaalam wa Misitu ambae pia anafanya kazi na  Mama Misitu kupitia Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Cassian Sanga akiendesha mjadala wa mada ya kwanza ya usimamizi  endelevu wa rasilimali za misitu nchini.


Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA)  leo imeanza mkutano wake Mkuu wa Siku mbili ambao kwanza umeanza na Warsha ya siku moja ya wadau wote wa mtandao huo. Wajum,be na wadau wa Mjumita kesho Agosti 18, watafanya mkutano mkuu ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa huku Kauli mbiu ya mwaka huu katika Mkutano huo unaofanyika mkoani Morogoro ikiwa ni 'TUCHAGUE VIONGOZI WATAKAO TETEA USIMAMIZI ENDELEVU WA MISITU".

Mtandao huo umeandaa rasimu maalum ambayo wanakusudia kuigawa kwa wagombea wa  nafasi mbalimbali za uongozi pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuwa katika mikutano yao ya kampenzi itakayoanza Agosti 22 mwaka huu nchini  kote wananchi wasisite kuwauliza wagombea hao juu ya mstakabali wa  rasilimali za misitu zilizopo katika maeneo yao  kwa kuzingatia kuwa  misitu ni uhai kwa maisha ya mwanadamu.
Elias Monga, Meneja mradi wa MJUMITA akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.
 Hii ndio kauli mbiu ya Mujumita katika Mkutano wake wa 15 mwaka huu unaofanyika mjini Morogoro.
 Mmoja wa Maafisa Misitu akizungumzia mikakati ya uhifadhi misitu na namna bajeti Kuu ya Serikali inavyochangia fedha katika uendelezaji na usimamizi wa Misitu nchini. Maafisa Misitu kutoka Wilaya Mbalimbali wamealikwa kushiriki katika Warsha hiyo ambapo wamesema licha ya Halmashauri zao kutenga fungu kwaajili ya uendelezaji Misitu lakini hakuna fedha zilizoingizwa licha ya baadhi ya Halmashaurti kupata mapato mengi yatokanayo na misitu.
Mjumbe wa Bodi ya MJUMITA Kanda ya Mashariki, kutoka Kijiji cha Soga Kibaha Mkoani Pwani, Subira Juma akizungumza juu ya umuhimu wa kuwachagua viongozi walio na uwezo wa kutetea usimamizi endelevu wa Mazingira.
Mtoa mada ya ushiriki wa Wananchi katika Uchaguzi Mkuu
utakao fanyika Oktoba 25,2015 Pasience Mlowe kutoka Kituo cha Haki za 
Binadamu, akiwasilisha mada hiyo kwa washiriki wa warsha hiyo.

Mjumbe wa Bodi ya Mjumita Mstaafu, Juliana Mwenda akifafanua jambo kuhusiana na mkakati huo wa kuwashirikisha wagombea na kuwajengea uwezo wa ufahamu juu ya umuhimu wa utetezi wa rasilimali za misitu  
Baadhi ya washiriki wakifuatikia warsha hiyo leo ambapo mada mbalimbali zilitolewa ikiwa ni pamoja na ushiriki wa Wananchi katika uchaguzio Mkuu 2015, Uchaguzi Mkuu na changamoto za wakulima wadogo wadogo na Umuhimu wa Kiongozi bora katika kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali za misitu. SOURCE: Father Kidevu Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)