Pages

MH LOWASSA APITISHWA NA MKUTANO MKUU WA CHADEMA KUWA MGOMBEA URAIS TANZANIA NA DKT JUMA HAJI KUWA MGOMBEA MWENZA

 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (wa nne kulia) akiwa ameshikana mikono na Mgombea wa Urais alieteuliwa na chama hicho, Mh. Edward Lowassa (wa tatu kulia) pamoja na Mgombea Mwenza wake, Mh. Dkt. Juma Haji Duni (mwenye suti nyeusi) pamoja na wanachama wapya wa Chama hicho, wakati wakitambulishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) akimpongeza Mgombea wa Urais alieteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa mara baada ya kupitishwa bila kupingwa na Mkutano Mkuu kuwa Mgombea wa Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Katikati ni Mgombea Mwenza, Mh. Dkt. Juma Haji Duni.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akimpongeza Mgombea wa Urais wa CHADEMA, Mh. Edward Lowassa mara baada ya kupitishwa bila kupingwa na Mkutano Mkuu wa Chama hicho kuwa Mgombea wa Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Katikati ni Mgombea Mwenza, Mh. Dkt. Juma Haji Duni.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akitoa hotuba yake wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
Crdt Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)