Pages

MASHIRIKA MATANO YA KITAIFA NA KIMATAIFA(FOS) YAUNGANA KWA PAMOJA KUTOA ELIMU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015

Wasemaji kutoka Mashirika Matano Kutoka kushoto ni Msemaji kutoka LHRC,OXFAM, Restless Development, BBC na VSO
  Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa Oxfam Jane Foster ambao pia ndio waandaaji wa Mkutano huu na waandashi wa Habari akieleza kwa kina nia ya Mkutano huo ambao lengo kuu ni kuzungumzia maswala ya Uchaguzi kuwa kila mtu anahaki ya kupiga kura.
  Hellen Kijo Bisimba ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa
kituo cha sheria na haki  za binadamu (LHRC) (Kushoto) akiongea jinsi walivyo endesha zoezi zima la kusimamia uandikishaji wa Daftari la uandikishaji wa wapigakura la kudumu BVR na ushiriki wao kwa ujumla.
Meneja wa Programu kitengo cha Governance kutoka Oxfam Bi.  Betty Malaki  akiendelea kutoa utaratibu katika Mkutano huo.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Restless Development Bi. Rahma Bajun ambao jukumu lao limelenga sana kwa vijana , akitoa taarifa ya Jinsi walivyo washirikisha vijana katika kuwahimiza na kuwapa elimu ya uchaguzi na kupiga kura ambapo wanafanya kazi hasa katika mikoa ambayo ipo Pembezoni ambayo ipo 11 .
 Mwakilishi kutoka Shirika la Utangazaji la BBC Bi.Neema Yobu akielezea jinsi wanavyo simamia na kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari nchini, kutoa elimu ya uandishi bora wa Habari za kipindi cha uchaguzi mkuu 2015.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Innovation Skills Results Bw. Jean Van Wetter akieleza jinsi wanavyohusika kwa ukaribu kabisa hasa katika upande wa vijana wa umri wa kati kuwaelimisha juu ya umuhimu wa Uchaguzi ambapo alisisitiza kuwa vijana wanatakiwa kupewa mapema elimu hii ili wanapokuwa wafahamu umuhimu wa uchaguzi.
 Mmoja wa wasemaji kutoka VESO Bi. Lina Muro akisisitizia Jambo<!--[if gte mso 9]>
Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa katika Mkutano huo.

Umoja wa Mashirika Matano yanaounda ushirika wa Fahamu,Ongea Sikilizwa(FOS) ambayo ni Oxfam,BBC Media Auction, Legal and Human Rights Centre, Restless Development, and VSO leo wamekutana na waandishi wa Habari kwa ajili ya kuzungumzia mambo Mbalimbali yanayohusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2015 na kueleza malengo ya muungano huo.
Akizungumza Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Bi. Jane Foster ambao ndio waandaaji wa Mkutano huo na waandishi wa Habari alisema kuwa Lengo kubwa la Umoja huo ni kusisitiza na kuwaelimisha wananchi wote kwa ujumlan juu ya Uchaguzi mkuu 2015 ambapo Oxfam wao jukumu lao kubwa ni kuwahimiza wanawake na wasichana wadogo  kuelekea uchaguzi Mkuu kama wapiga kura, na ili kuyafikia makundi yote haya waliandaa na wanaendesha Midaharo mbalimbali, kuunda makundi ya wanawake na zaidi wanatumia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter kuwapa taarifa juu ya uchaguzi.
BBC kwa upande wao wanajukumu la kusimamia mashirika mbalimbali ya utangazaji Nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na kanuni za uandishi bora wa Habari za uchaguzi Mkuu 2015 

Nao kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambao walikuwa na jukumu la Kusimamia zoezi zima la uasdikishaji wa wapiga Kura ambapo walikuwa na watu 165 nchi nzima wakiangalia na kuangalia makosa yaliyojiokeza na kupeleka Maoni yao sehemu husika, na pia katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 wameandaa kitengo maalumu cha Teknolojia ambacho kitasimamia uchaguzi wote.



Wakati huo huo restless Development wamewafundisha vijana 22 ambao wamesambazwa katika mikoa 18 Nchi nzima kwa lengo kuwakusanya vijana katika makundi mbalimbali kwa nia ya kuwapa elimu kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2015, sambamba na hapo wamelenga kuwapa elimu viongozi wa ngazi za chini yaani Wilaya, Pia vyombo vya habari pamoja na Polisi, ambapo kwa sasa Shirika hili linaandaa ajenda mbalimbali kuelekea uchaguzi Mkuu 2015.


Pia Shirika la Voluntary service Overseas nao wameendesha mafunzo kwa viongozi wa chini, viongozi wa Dini katika mikoa Nane(8) Tanzania ambao wanashirikishwa moja kwa moja katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Mikoa hiyo ni Pamoja na Lindi, Mtwara, Kagera na Mikoa mitano Zanzibar ambayo ni Wete,Chakechake, Unguja, Makokotoni na Unguja Kaskazini. wakieleza juu ya uchaguzi Mkuu 2015.

Akizungumza
na waandishi wetu mmoja wa wakurugenzi
wa mashirika hayo, Hellen Kijo Bisimba ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa
kituo cha sheria na haki  za binadamu
(LHRC), alisema kuwa moja kati ya mapungufu yaliyoonekana katika uchaguzi huo
ni kuwepo kwa imani potofu hasa katika kipindi cha kujiandikisha kwa kutumia
mashine za BVR ambapo wananchi wengi hasa wa vijijini walikuwa na dhana kuwa
mashine hizo huweza kuwapima watu Ukimwi na wengine kushikana uchawi hasa wale
ambao alama zao za vidole hazikuonekana au zilipatikana kwa shida.
Katika mikoa
mingine mkurugenzi huyo alisema kuwa watu walifikia mbali zaidi na kuaminishana
kuwa mashine hizo ni za Freemason na makundi ya wanyonya damu mambo ambayo
yalichangia wengi wao wasishiriki zoezi zima la uandishaji na kuongeza kuwa
changamoto zote hizo walizibaini na kuzifikisha kwa tume.
“Kuna maeneo
walihamasishana kabisa kutojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura
hasa kwa njia BVR wakidai kuwa ni ya Freemason au wanyonya damu huku wengine
wakishikana uchawi kwa kuwa alama zao za vidole hazisomi kwenye mashine hizo. Hizo
zote ni changamoto na tumezifiksha kwenye tume,” alisema Bi Hellen na kuongeza
kuwa hata hivyo muamko wa vijana mwaka huu ni mkubwa sana jambo linalotoa
tafsiri kuwa uchaguzi huu utakuwa shirikishi kuliko hapo awali.


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)