Pages

Majaji wa TMT 2015 wageni wa TMT house

Majaji wa Shindano la TMT wakiwa ndani ya Mjengo wa TMT kwaajili ya kuwatembelea washiriki waliobaki mjengoni
Washiriki wa Shindano la TMT 2015 wakipitia muswada yaani script kabla ya kuingia kazi kwaajili ya kushoot filamu fupi
Washiriki wakiwasikiliza majaji kwa makini

Katika maandalizi ya short film wiki hii washiriki wamepata wageni katika nyumba yao kule Masaki,wageni hao ni Majaji wa shindano la Tanzania Movie Talents TMT  2015 Jaji Mkuu Roy Sarungi,Jaji Monalisa,Jaji Rich Rich Single Mtambalike.

Majaji hao walipata wasaha wa kuzungumza na washiriki wa TMT 2015 kwa kuwapa ushauri jinsi ya kufanikiwa katika maisha yao kwa kuwa wenye nidhamu na wanyenyekevu katika sanaa bila kutaka kukumbilia mafanikio,kuwa wabunifu watakapotoka kwenye mashindano ya TMT kwa kusema kidogo walichokipata ni shule au mtaji tosha wa kuendeleza sanaa yako kama ajira.

Rich Rich au Single na Mtambalike na Monalisa wakizungumza nao walisema wao miaka ya nyuma wakati wanaanza sanaa katika vikundi kabla ya kuanza kuonekana ITV miaka ya nyuma walipitia wakati mgumu sana kwa kutembea umbali mrefu kufuata sanaa au kushinda njaa ikiwa ni sehemu ya kutafuta kitu wanachopenda,mwisho wa siku leo wameweza kufika hapa walipo na kuwa wasanii wakumbwa nchi,walisema Rich Rich na Monalisa.

Washiriki waliongia katika jua la utosi (Danger zone)kwa wiki hii ni Nadhifa Haruna, Mohamed Massanga, Sadam Nawanda, Naomi Chuwa, Catherine Nicholaus na Rachel Michael

Mpigie kura Mshiriki umpendae ili kutoka katika jua la utosi (Danger zone) aendelee kubaki katika mashindano ya TMT 2015 na kumpa nafasi zaidi ya kushinda milioni 50. Andika TMT acha nafasi, namba ya mshiriki kisha tuma kwenda 0784367738.

‪Nadhifa Haruna 01,Aisha Katabazi 02,Kalombo Amboni 04,Dennis Laswai 05,Tomluck Stephan Shukuru 06,Catherine Nicholaus 07,Titus Maridhia 08,Daniel Lufingo

Jackson Sakumi 12,Naomi Chuwa13,Sadam Nawanda 14,Mohamed Massanga 15,Saidi Bakari Mbelemba16,Rachel Michael 17.

Usikose kutazama kipindi cha TMT kinachoruka kila Jumapili saa 3:30 usiku,marudio Alhamis saa 5:30 usiku na Jumamosi saa 7:00 mchana pekee!

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)