Pages

MAGUFULI ASAINI HATI YA KIAPO YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAKAMA KUU JIJINI DAR LEO

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli  akikabidhi hati ya Kiapo mapema leo mchana kwa Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Sekieti Kihiyo (katikati). Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam  Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
 Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli akisaini hati ya Kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
 Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Jaji Sekieti Kihiyo mara baada ya  kusaini hati ya kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa ndani ya moja ya chumba cha Mahakama Kuu wakirekodi tukio la Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli sambamba na mgombea Mwenza,Samia Suluhu Hassan walipokuwa wakisaini hati ya Kiapo mapema leo mchama Mahakamani Hapo mbele ya Jaji  Sekieti Kihiyo. 
 Mgombea urais wa chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nje ya jengo la Mahakama Kuu mara baada ya kusaini hati ya Kiapo mapema leo mchana.Hati hiyo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini mahakamani hapo jijini Dar es Salaam. PICHA NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)