Pages

MAGUFULI AHIDI KUANZISHA MAHAKAMA YA MAFISADI NA WALA RUSHWA IWAPO ATACHAGULIWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano.

Dkt Magufuli amesema kuwa serikali atakayoingoza atakapopata ridhaa ya kuingia Ikulu,itazifanya huduma za Afya kuwa bora na kuwabana wahudumu wa afya wenye tabia ya kuchukua dawa na kuziuza kwa watu binafsi.

Magufuli ambaye yupo katika mikoa ya Nyanda za juu kusini katika kampeni ya kusaka nafasi ya kuwa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema suala la afya litakuwa moja ya ajenda zake muhimu atakapoingia madarakani.

Katika hatua nyingine Dkt Magufuli amewaleza wananchi kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuiongoza Tanzania,atahakikisha anaanzisha mahakama maalumu ya Mafisadi na Wala rushwa. PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA.
 Mbunge wa zamani wa jimbo la Kyela Mzee John Mwakipesile akimpigia debe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt  John Pombe Magufuli wakati mgombea huyo alipofika jimboni humo kuomba kura za wananchi ili wamchague kuwa rais.Mzee Mwakipesile amesema kuwa anamuunga mkono Dkt Magufuli na atahakikisha anashiriki kikamilifu kuhakikisha mgombea huyo anaibuka na ushindi kwa kishindo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela Dkt Harrison Mwakyembe akimpigia debe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jionu ya leo.
  Naibu Waziri wa Fedha Mh Mwigulu Nchemba akihutubia katika  mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya,ambapo Mwigulu aliwaomba wananchi hao waliojitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na hatimae aweze kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano kwa sababu ana sifa zoto za kuongoza nchi.
 Maelfu ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Nzovwe Mbeya jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao.
 Naibu Waziri wa Fedha Mh Mwigulu Nchemba akihutubia katika  mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya,ambapo Mwigulu aliwaomba wananchi hao waliojitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na hatimae aweze kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano kwa sababu ana sifa zoto za kuongoza nchi.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano,Magufuli amewaambia wananchi hao kuwa atahakikisha  huduma za afya zinaimarishwa ipasavyo,katika suala la Elimu Magufu aliwaeleza Wananchi kuwa iwapo watamchagua katika nafasi hiyo ya Urais atahakikisha elimu kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne itatolewa bure,aidha pia amewataka Watanzania kuwa wamoja katika kuhakikisha wanailinda na kuitunza amani iliyopo nchini. 
 Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya. 
 Wafuasi na wapenzi wa chma cha CCM wakishangilia 
Maelfu ya Wananchi waliokusanyika katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo.
 Jicho la samaki katika ubora wake kwenye mkutano wa kampeni za CCM katika viwanja vya Nzonvwe mjini Mbeya.
 Mmoja wafuasi wa chama cha chadema ambaye aliikabidhi kadi yake kwa Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli na kutanganza kuhamia chama cha CCM,katika mkutano wa kameni uliofanyika katika uwanja wa Tandale,Tukuyu mjini wilayani Rungwe
 Baadhi ya Wananchama kadhaa wa Chadema wakiwa katika picha ya pamoja na Dkt Magufuli mara baada ya kutangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na ccm
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi waliokuwa wamefika katika uwanja wa Tandale mjini Tukuyu kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Baadhi ya wananchi wa mji wa Kiwila wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsikiliza na kumuona mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akipita kuelekea wilayani Kyela kwenye mkutano wa kampeni.
 Heka heka za wafuasi wa CCM
 Wananchi wa Kyela wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa John Mwakangale mjini Kyela,kwa ajili ya kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye mkutano wake wa kampeni mjini humo.
 Dkt Magufulia akiwahutubia wananchi wa Kyela mjini Ipinda



 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa
jimbo la Kyela kwa  wananchi wa mji wa Ipinda wilayani Kyela wakati
alipofika katika mji huo kufanya mkutano wa kampeni, Dr. John Pombe
Magufuli amewaomba wananchi wa Kyela kumpa kura za ndiyo Dr. Harrison
Mwakyembe ili  aweze kumtumia mara atakapochaguliwa na kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania


 Dkt Magufuli akiwapungia wananchi wa Tukuyu mjini alipowasili mjini humo kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni.
 Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni 
 Mh.David Mwakyusa akimwombea kura mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wananchi ili apate ridhaa ya kuwatumikia wananchi akiwa Ikulu.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tukuyu mjini kwenye kutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tandale mjini gumo jioni ya leo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)