Pages

KUMBUKUMBU YA MIAKA 3 YA MWENYEKITI WA GLOBAL PUBLISHERS MZEE BUKUMBI YAFANYIKA BUPANDWAMHELA LEO

Picha ya marehemu James Bukumbi ikiwa mbele ya waumini wakati wa ibada leo.
Watoto wa marehemu mzee Bukumbi, Eric Shigongo (wa kwanza kulia), Marsha Bukumbi (wa kwanza kushoto) na baadhi ya ndugu wakiweka shada la maua katika kaburi la baba yao.
Eric Shigongo akielezea historia ya baba yake, marehemu James Bukumbi wakati wa ibada ya kumbukumbu ya miaka mitatu tangu kifo chake.
Padri George Nzungu ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mt. Kizito, Kabila, Magu akiongoza ibada ya kumbukumbu ya miaka mitatu ya mzee Bukumbi.
Wanafamilia ya James Bukumbi wakiwa katika ibada hiyo ya kumbukumbu.
Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika ibada ya kumbukumbu ya miaka mitatu ya mzee Bukumbi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo ambaye ni mmoja wa watoto wa mzee Bukumbi akitoa sadaka wakati wa ibada hiyo.
Mmoja wa wakurugenzi wa Global Publishers, Marsha Bukumbi ambaye pia ni mtoto wa marehemu akishiriki ibada ya kumbukumbu.
Lydia Bukumbi ambaye naye ni mmoja wa wakurugenzi wa Global Publishers naye akitoa sadaka yake wakati wa ibada ya leo.
Mhariri wa Gazeti la Championi Jumamosi, Elius Kambili naye kitoa sadaka yake wakati wa ibada ya leo.
Wanakwaya wakiimba wakati wa ibada hiyo.
 Padri George Nzungu (kulia) akisaidiana na Padri Ibrahimu Ngassa kuongoza ibada hiyo.
Ibada ikiendelea nyumbani kwa marehemu mzee James Bukumbi.
Safari ya kuelekea makaburini.
Wanafamilia wakiwa katika kaburi la mzee Bukumbi.

Ibada ikiendelea katika kaburi la mzee Bukumbi.
Wanafamilia wakiwa na shada la maua wakati wa ibada ya kumuombea mzee Bukumbi.
Mapadri wakiweka shada la maua katika kaburi la mzee Bukumbi wakati wa ibada hiyo.
Masista nao wakiweka shada la maua.
Diwani wa Kata ya Bupandwamhela, Masumbuko Machimwi (wa kwanza kulia) na Diwani wa Kata ya Katwe Kanyumi Henry (wa pili kulia) wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mzee Bukumbi.
Baadhi ya wajukuu wa kike wa mzee Bukumbi wakiweka shada la maua kwenye kaburi la babu yao.

Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers wakiweka shada la maua katika kaburi la mzee Bukumbi.
KUMBUKUMBU ya miaka mitatu tangu kufariki kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Publishers & Gen. Enterprises Ltd, James Bukumbi imefanyika leo katika kijiji cha Bupandwamhela, wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Ndugu, jamaa na marafiki wameungana na familia ya marehemu James Bukumbi katika ibada ya misa ya kumbukumbu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Bupandwamhela.
Ibada hiyo ya kumbukumbu imeongozwa na Padri George Nzungu ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mt. Kizito, Kabila, Magu akisaidiana na Padri Ibrahimu Ngassa.
Katika mafundisho yake, Padri Nzungu amewaasa waumini kumuweka Mungu mbele katika maisha yao ya kila siku na kutenda matendo mema huku akitumia muda mwingi kuwafariji wanafamilia, ndugu, jamaa na wanakijiji waliohudhuria kuwa marehemu James Bukumbi yuko mahali salama na wazidi kumuombea.
(PICHA: DENIS MTIMA, BRIGHTON MASALU NA IDD MUMBA / GPL, BUPANDWAMHELA)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)