Pages

KIPINDUPINDU CHAENDELEA KUTESA JIJINI DAR ES SALAAM

 Muuguzi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Nusura Kessy (kushoto), akiwaelekeza wauguzi wa saidizi wake namna ya kuchanganya dawa maalumu ya kuondoa vijiji vinavyoweza kuwa vya ugonjwa wa kipindupindu katika kambi ya wagonjwa walioathiriwa na ugonjwa huo iliyopo Zahanati ya Mburahati Dar es Salaam leo asubuhi. Katika kambi hiyo kuna wagonjwa 21 kati yao watoto ni 7.
 Vyombo vikiwekwa kwenye dawa.
 Muuguzi Msaidi wa Zahanati ya Mburahati, Maimuna Pazi (kushoto) na Mlinzi wa Zahanati hiyo, Abdallah Mbagala wakisaidiana kuweka dawa maalumu ya kuzuia kuenea kwa vijidudu vya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu katika vyombo walivyoletewa chakula na ndugu zao katika kambi ya matibabu kwa wagonjwa walioathiriwa na ugonjwa huo iliyopo katika Zahanati ya Mburahati Dar es Salaam leo asubuhi.
Dawa hiyo maalumu ikiwekwa katika vyombo vya kutumia.

Na Dotto Mwaibale

HALI ya ugonjwa wa kipindupindu ulioikumba maeneo kadhaa ya jiji bado inaonesha ni tete kufuatia idadi ya wagonjwa huo kuongezeka kutoka watu 34 na kufikia 43.

Hayo yamebainishwa na Muuguzi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni ambayo imeathiriwa na ugonjwa huo, Nusura Kessy wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi.

Kessy ambaye anasimamia kutoa huduma katika kambi ya wagonjwa iliyopo Zahanati ya Mburahati alisema mpaka jana asubuhi kulikuwa na wagonjwa 21 kati yao watoto ni saba na wagonjwa 10 wameruhusiwa kurudi majumbani mwao baada ya hali zao kuimarika.

"Hali bado sio nzuri kwani tunaendelea kupokea wagonjwa kutoka Hospitali ya Mwananyamala hata hivyo uwezo wa vyumba vya kulaza wagonjwa ni watu 16 tu" alisema Kessy.

Alisema kutokana na changamoto hiyo wameomba mahema ambayo yatafungwa nje ya zahanati hiyo kwa ajili ya kusaidia ongezeko hilo la wagonjwa.

Kessy alitunmia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuzingatia usafi hasa baada ya kutoka kujisaidia kunawa kwa kutumia maji ya moto na kuto kula vyakula holela pamoja na kuchemsha maji ya kunywa.

Muuguzi huo pia alitoa mwito kwa wananchi pale wanapo muona mtu anatapika na kuharakisha kutoa taarifa mapema na kumpeleka mgonjwa hospitali kwa matibabu.

Alisema kuwa kati ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo kati yao ni walifariki wakiwa majumbani na njiani wakati wakipelekwa hospitali wakiwa katika hali mbaya baada ya kucheleweshwa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)