Pages

Kenya yasitisha mkataba CNN kutangaza utalii

CNN ilidai Kenya ni kitovu cha ugaidi.
Halmashauri ya Utalii nchini Kenya imesema kuwa imefuta kandarasi ya matangazo ya kibiashara na televisheni ya Marekani CNN kwa sababu ya mzozo kuhusu ripoti iliyotangazwa na shirika hilo kuihusu Kenya. Wakenya wengi walikasirishwa na ripoti ya CNN iliyodai taifa la Kenya ni kitovu cha ugadi muda siku chache kabla ya ziara ya rais Obama nchini humo.
Wakenya walirusha cheche za maneno kwenye twitter kuihusu CNN
Halmashauri ya Utalii nchini Kenya ilikuwa imeipa CNN kandarasi ya kima cha dola milioni 100 kutangaza vivutio vya utalii nchini humo. Lakini sasa mkataba huo umesitishwa kwa kipindi cha mwaka mmoja. Mkataba huo ulijumuisha matangazo ya kibiashara kwenye runinga na kupitia mtandao wa CNN.
Msemaji wa halmashauri hiyo amesema kuwa bado hawajapata jibu kutoka CNN na sasa wanashauriana na serikali ya Kenya. Mada ya mazungumzo kwenye twitter #SomeoneTellCNN ilikuwa maarufu sana nchini Kenya baada ya ripoti hiyo kupeperushwa na CNN. Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery aliitaka CNN kuomba msamaha.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)