Pages

FILAMU MPYA YA WAKE-UP KUZINDULIWA AGOSTI 30, 2015 JIJINI DAR ES SALAAM

 Muandaaji wa Filamu ya Wake-Up, Manaiki Sanga (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu filamu hiyo mpya inayotarajiwa kuzinduliwa Agosti 30, 2015. Kulia ni msanii wa filamu, Farida Sabua 'Mama Sonia na Salim Ahmed 'Gabo'.
 Msanii wa filamu, Taiya Odero (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Meza kuu. Kutoka kulia ni Taiya Odero,  Farida Sabua 'Mama Sonia,  Muandaaji wa Filamu ya Wake-Up, Manaiki Sanga , Salim Ahmed 'Gabo na Kaushik Surelia.
 Msanii wa filamu, Salim Ahmed 'Gabo' (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Msanii Farida Sabua 'Mama Sonia (kulia), akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

WATANZANIA na wadau wa filamu wameomba kuunga mkono filamu mpya ya Wake-up ambayo inatarijiwa kuzinduliwa Agosti 31, 2015 jijini Dar es Salaam.

Mwito huo umetolewa na muandaaji wa filamu hiyo Manaiki Sanga wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu filamu hiyo.

"Filamu hii ni ya aina tofauti na filamu ambazo zimefanywa hapa nchini kwani imewashirikisha mastaa wa bongo movie 31 na imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu" alisema Sanga.

Alisema maudhui ya filamu hiyo yamehusu zaidi familia na inaweza kuonwa na watu wa rika lote na imezingatia maadili na utamaduni wa kitanzania.

Sanga aliwataja baadhi ya wasanii waliocheza filamu hiyo kuwa ni Mzee Majuto, Irene Uyowa, Hemed PHD, Quick Rock, Frola Mvungi, Asha Boke, Mama Sonia, Gabo, Prince Kas na wengine wengi. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)