Pages

CHADEMA MOSHI MJINI WATANGAZA ILANI YA UCHAGUZI YA JIMBO LA MOSHI MJINI.

Meneja Kampeni wa mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini kupitia Chadema na UKAWA,Jafary Michael ,Bw Raymond Mboya akifanya utamburisho mbele ya wanahabari wa mkutano wa mgombea huyo na wanahabari uliofanyika katika Hotel ya Keys.
Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro ambao ni wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini wakiwa katika kikao na mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini kupitia Chadema na UKAWA,Jafary Michael.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini aliyemaliza muda wake ,Philemoni Ndesamburo(Chadema) akizungumza na wanahabari (hawako pichani) wakati wa kikao cha mgombea Ubunge wa jimbo hilo kueleza Ilani ya chama chake katika ngazi ya jimbo hilo.
Baadhi ya wanahabari.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akizungumza katika kikao hicho kuelezea kilchomo katika ilani ya Chadema ngazi ya jimbo la Moshi mjini.
Baadhi ya wanahabari.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

ILANI YA CHADEMA
KATIKA MANISPAA YA MOSHI.

1.      ELIMU:
A.     ELIMU YA AWALI:
·       
Kuimarisha
madarasa ya awali.
·       
Upatikanaji wa
walimu wa awali.

B.      ELIMU YA MSINGI:
(i)               
Kuongeza matundu ya vyoo katika shule za msingi
ndani ya Manispaa ya Moshi.
(ii)             
Kujenga silos katika shule mbalimbali za msingi ya
kuhifadhi nafaka za shule.
(iii)           
Kuongeza nyumba za walimu.
(iv)            
Kuongeza madarasa na kukarabati  yaliyopo.
(v)              
Kusaidia kulipia michango ya chakula kwa watoto
yatima na wanaotoka familia duni
(vi)            
Kuimarisha elimu ya computer katika shule zetu za
msingi.
(vii)          
Kuongeza mtandao wa maji safi kwa shule za msingi.

C.      ELIMU YA SEKONDARI:
·       
Kuongeza matundu ya vyoo
·       
Kuongeza na kuimarisha miundombinu ya vyumba vya
maabara.
·       
Kuongeza vyumba vya kulia chakula (mabwalo).
·       
Kujenga maktaba katika shule za sekondari.
·       
Kupandisha daraji baadhi ya shule za kawaida kuwa za
kidato cha tano na sita.
·       
Kuhakikisha familia duni na za watoto yatima
zinasaidiwa michango mbalimbali ya shule.


(2) AFYA:
·       
Kusukuma upatikanaji wa hospitali ya Wilaya.
·       
Kuimarisha vyumba vya upasuaji katika vituo vya afya.
·       
Kuboresha zahanati.
·       
Kujenga vyumba vya kuhifadhia maiti katika vituo vya
afya.
·       
Kujenga uzio katika vituo vya afya na zahanati ili
kudhibiti usalama wa wagonjwa.
·       
Kusukuma kusimamia kwa sera ya matibabu ya bure kwa
wazee na watoto chini ya miaka mitano.
·       
Kuongeza na kuimarisha vyumba vya kuzalishia.
(labour ward)
·       
Kuongeza nyumba za waganga wa vituo.

(3) MAJI:
·       
Kuongeza mtandao wa maji safi na maji taka kwa
kushirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka.((MUWSA)
·       
Mh: Kata ya Kiboriloni, Longuo B na Rau.

(4) Makundi
maalum:
·       
Kuboresha miundombinu ya makundi maalum katika
majengo ya serikali
·       
Kuimarisha na kuboresha miundo mbinu ya shule za
watu wa makundi maalum.
·       
Kushirikiana na vyama vya watu wenye ulemavu
·       
Kushirikiana na Asasi za kiraia zinazohudumia makundi
maalum katika jamii

(5)
MIUNDO MBINU:
·       
Kuongeza mtandao wa barabara za lami kwenye maeneo
ya katikati ya mji na
Kata za
pembezoni.
·       
Kupandisha barabara za kiwango cha vumbi kwenda
kiwango cha changarawe(moramu)
·       
Kuimarisha barabara mbalimbali ndani ya Kata na
Mitaa yake katika manispaa ya Moshi.
·       
Kujenga na kuimarisha mfereji wa maji ya mvua katika
manispaa ya Moshi ili kulinda barabara za Manispaa.
·       
Kujenga vivuko na kumalizia madaraja ndani ya
Manispaa ya Moshi.
·       
Kuongeza na kuimarisha mtandao wa taa za barabarani.

 (6) UCHUMI:
(A) AJIRA:
(i) Tutaendelea kuboresha ajira zisizo rasmi (informal sector) ili ziwezeshwe kurasimishwa.
·       
Kutenga maeneo rasmi
·       
Kuzuia matumizi nguvu kwa wajasiriamali wakiwepo
wamachinga wadogo.
·       
Kuwapa elimu
·       
Kuwathamini wafanyabiashara sekta muhimu katika kukuza uchumi wa Moshi.

(ii) Kuendelea kuviwezesha vikundi vya vijana na kinamama kwa kutumia fedha za mfuko wa  vijana na kina mama.


(iv) Kuendelea kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya vikoba na saccos na kuimarisha       vilivyopo.

(v) Kuendelea kusukuma Serikali Kuu ili kufufua viwanda vilivyo binafsishwa kwa ajili ya kutoa ajira kwa wananchi wa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.

(vii) Kuendelea kujenga mazingira rafiki na mahusiano mazuri na sekta binafsi ili kusukuma na kuharakisha uwekezaji katika mji wa Moshi kwa ajili ya kuongeza ajira. (Service levy)

(viii) Kulinda na kusimamia matumizi sahihi ya rasilmali za halmashauri ikiwepo kutafuta wawekezaji katika maeneo ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

(xi)  Kuendelea kuongeza mapato ya Halmashauri mwaka hadi mwaka kwa kuboresha mfumo wa takwimu za ukusanyaji wa mapato. (Data base)

(B)UTALII:
(i) Kuangalia uwezekano wa kuongeza vivutio vya watalii katika Manispaa ya Moshi ikiwepo kuendeleza mazungumzo na Wizara ya Mali Asili na Utalii ya kuingia ubia na Manispaa ya Moshi ya kuboresha msitu RAU.

(ii)  Kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika hoteli za kitalii za nyota tatu mpaka tano ili kuongeza idadi ya watalii wanaolala katika mji wa Moshi.

(iii) Kuendelea kusukuma uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Moshi (Moshi Airport) uweze kufanya kazi kwa ufanisi .

(iv) Tutaendelea kutetea maslahi ya wapagazi na kushirikiana na vyama
vyao.

(C) MCHAKATO WA MANISPAA YA MOSHI KUWA JIJI LA MOSHI.
Kuendelea kumshawishi Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atoe tamko la Moshi kuwa jiji baada ya kukamilisha mchakato wote kwa mujibu wa sheria.

(D)KILIMO:
 kuendelea kuboresha kilimo cha mjini (Urban agriculture) kwa kuimarisha kilimo cha kisasa katika ukanda wetu wa kilimo ndani ya Manispaa ya Moshi ikiwa ni pamoja na uvuvi na ufugaji.

(E) MASOKO:
 Kusimamia uboreshaji masoko ya manispaa ili yafanye kazi kwa ufanisi.

(7) MICHEZO:
(a) Kuendelea kuimarisha viwanja vya michezo katika Manispaa ya Moshi.

(b)  Kuimarisha ushindani wa wanamichezo katika Kata za manispaa ya Moshi ili kuibua vipaji mbalimbali katika michezo ya aina tofauti.

(c) Kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangia timu za michezo tofauti
katika Manispaa ya Moshi ili kupata timu za michezo mbalimbali zitakazowakilisha manispaa katika michezo ya kitaifa.

(d) Halmashauri ya Manispaa ya Moshi itaandaa sera za michezo inayooanisha michezo na uchumi na michezo na ajira ili kuondoa dhana kuwa michezo ni burudani tu.

(8) MAZINGIRA:
(a) Kuhamasisha upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali ya Manispaa.

(b) Kutunza vyanzo vya maji.

(c) Kuendeleza usafi wa mji wa Moshi;

 (i)Kutoa elimu kwa wananchi wa Moshi

 (ii) Kuhamasisha watu kutenga takataka katika vyanzo (separation at source)
(iii) Kufanya takataka kuwa rasilimali na sio uchafu hivyo kuzalisha ajira.
(iv) Kutengeneza gesi asilia (Bio gas) na  mbolea ya mboji
(v)  Kuongeza vitendea kazi kama magari na vinginevyo.
(vi) Uboreshaji wa dampo kuu (land field).

(9)
ARDHI NA MIPANGO MIJI:
(a) Upimaji wa maeneo ya makazi kwa kuondoa ujenzi holela.

(b) Kupima maeneo ya halmashauri ya manispaa ya Moshi  kwa ajili ya kupata hatimiliki.

(c) Kusimamia ujenzi unaoendelea na mpango kabambe wa uendelezaji wa
mji wa Moshi (Master plan) ya mwaka 2001)

(d) Kuzuia uvamizi wa maeneo ya wazi

(e) Kutengeneza na kusimamia mpango kabambe wa miaka kumi na tano wa kuendeleza mji wa Moshi, utahusisha Kata za Majengo, Bomambuzi, Korongoni, Kiusa,Mawenzi na Bondeni.

(f) Kukabiliana na migogoro ya ardhi inayosababishwa na idara ya
ardhi ikiwepo kugawa kiwanja kimoja zaidi ya mtu mmoja.

(g) Kusukuma upatikanaji wa hati miliki kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)