Pages

BODI YA USAJILI WA WAHANDISI (ERB) YAELEZEA MAFANIKIO YAKE

 Msajili Mkuu wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB), Mhandisi Steven Mlote.
 Msajili Mkuu wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Steven Mlote (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya bodi hiyo na serikali ya awamu ya nne kwa kipindi cha mwaka 2005-2015. Kulia ni Msajili Msaidizi wa bodi hiyo, Mhandisi Benedict Mukama na na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani wa ERB, Vicentus Vedasto..
Mkutano na wanahabari ukiendelea.



Na Dotto Mwaibale

BODI ya Usajili ya Wahandisi nchini (ERB) imewafutia vibali vya 
usajili wahandisi 330 baada ya kubainika kukiuka taratibu za ufanyaji kazi wa bodi hiyo.


Hayo yalibainishwa na Msajili Mkuu wa bodi hiyo Mhandisi, Steven Mlote wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya bodi hiyo na serikali ya awamu ya nne kwa kipindi cha mwaka 2005-2015laam jana.

Mlote alisema kufutiwa vibali vya wahandisi hao imetokana na uchunguzi wao walioufanya katika vipindi tofauti na kubaini mapungufu makubwa katika kutekeleza majukumu yao ya  sekta ya ujenzi hapa nchini.

"Hatua hiyo ilifikiwa na bodi yetu baada ya kujiridhisha na kufikia maamuzi hayo baada ya kufanya uchunguzi wa kina" alisema Mlote.

Alisema kufanyakazi za uhandisi chini ya kiwango ni hatari na ndio maana waliamua kuchukua tahadhari ya kuwafutia vibali wahandishi hao.

Mlote aliongeza kuwa mbali na hatua hiyo ERB imezifungia kampuni 32 za wahandisi kampuni, 17 ni za kizalendo na 15 ni za kigeni.

Alifafanua kuwa kwa kipindi chote hicho wamekuwa wakidhibiti mienendo shughuli za kihandisi nchini huku akiziangalia kwa 
umakini kampuni zilizopata usajili ziwe na utendaji mzuri.

Mlote alisisitiza kuwa ni marufuku kwa kikundi cha watu au mtu 
kufanya shughuli za Kihandisi bila kusajiliwa na watachukuliwa 
hatua za kisheria kwa makosa hayo.

Katika miaka ya  karibuni Ujenzi ulio chini ya kiwango umesababisha maafa mengi na chanzo kikubwa ni Ujenzi ulio chini ya kiwango.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)