Pages

BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO YASHIRIKI NANENANE KITAIFA MKOANI LINDI

1
Mmoja wa wafanyakazi wa benki ya Maendeleo ya Wakulima, Geofrey Mtawa akizungumza na moja ya wadau waliotembelea banda lao katika maonyesho ya Nanenane.

Na Mwandishi wetu
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania inashiriki maonesho ya kilimo ya Nanenane kitaifa kwa mara ya kwanza mkoani Lindi mwaka huu kwa lengo la kutambulisha huduma zake kwa wadau wake wakuu, wakulima.

Katika maonesho hayo yaliyofunguliwa rasmi jana jumanne na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda, benki hiyo inatoa elimu na kujitambulisha kwa wakulima kwa kuwaelezea huduma zake zenye lengo la kuanzisha mtizamo mpya wa kukiendeleza kilimo kupitia kushirikisha wadau mbali mbali, kuangalia kila mnyororo wa thamani kwa ukamilifu wake, pamoja na kuwa na ubunifu katika kuchangia kifedha kwenye miradi ya muda mrefu, ya kati na muda mfupi kwenye sekta ya kilimo.
4
Akifungua maonesho hayo Waziri Mkuu Mh. Pinda, alisema kuwa Nanenane ni shamba darasa kwa wakulima kwa kuwa kupitia maonesho hayo wakulima watajifunza mbinu mbalimbali zenye kuongeza tija katika kilimo chao, na pia kujifunza wapi wanaweza kupata msaada kwa ajili ya kuinua kilimo chao sambamba na kujua namna wanavyoweza kutumia zana za kisasa ili kuongeza tija katika kilimo.

Benki ya Maendeleo ya Wakulima imeanzishwa maalum kwa ajili ya kuinua kilimo na itakuwa ikitoa huduma za uwezeshaji kwa wakulima na wafugaji kupitia wadau mbalimbali wa katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha kuwa pamoja na mambo mengine wakulima wa kitanzania wanafikiwa na zana za kilimo kama vile mbegu za kisasa, pembejeo, uwezeshaji wa vifaa vya usindikaji mazao ili kuongeza tija katika shughuli za kilimo.

Kwa wadau wanaotembelea banda lake hapa Nanenane, warapata fursa ya kuona vibanda vidogovidogo baadhi vikisheheni wakulima, wasindikaji na wauzaji wa bidhaa walizochakata wenyewe kutoka mashambani kwa upande mmoja lakini pia wako wadau wanaowezesha wakulima kama vile taasisi za utafiti wa mbegu za kilimo, wauzaji wa zana za kilimo kama SUMA JKT ili kuisaidia benki hiyo kufafanua namna itavyowezesha mfumo wa killimo na kuhakikisha kuwa mkulima anapata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.

Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe nane katika kilele cha maonesho haya ya Nanenane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimwa Jakaya Mrisho Kikwete.
3
Muonekano wa nje wa banda la benki ya wakulima la Nanenane.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)