Pages

''Afadhali kufariki baharini badala ya kuishi Libya''

Wahamiaji
''Afadhali kufariki baharini badala ya kuishi Libya''
Hivyo ndivyo alivyoniambia Christina mwenye umri wa miaka 24 wakati yeye na mumewe Samuel walipotolewa katika mashua iliyowaokoa ya MSF , Zaidi ni kuwa ni mja mzito.
Miaka mitatu iliopita walitoka nchini Nigeria na kuelekea Libya kwenye harakati za kutafuta maisha mazuri.
Alianzisha saluni iliyowahudumia wenyeji na wahamiaji.
Cristine
Wakati vita dhidi ya Gaddaffi vilipozidi alimbembeleza mumewe waende Uingereza.
Walifungwa macho wakati wa safari yote kutoka Benghazi hadi Tripoli ambayo ni safari ya Zaidi ya Kilomita 1,000 bila chakula au maji kabla ya kukabidhiwa kwa timu nyingine ya kusafirisha wahamiaji ambayo iliwasafirisha kwa masaa manne na kuwapeleka katika sehemu moja ya pwani isio na watu.
Huko walikutana na mashua tatu za kusafirisha wahamiaji
Waliagizwa kuingia katika boti hiyo kabla ya wasafirishaji hao kuipeleka baharini nyakati za usiku.
Cristine
'Walituambia tuendelee kusonga tutapata usaidizi', alisema
Baada ya masaa kadhaa ya kusafiri kwenye bahari, mashua hiyo ilianza kuvuja. Wanawake walianza kulia na kila mtu alihofia kuwa ndio mwisho wao.
Kwa bahati nzuri walipatikana na chombo cha uvuvi ambacho kiliwaokoa na badaaye kutuma ujumbe kwa chombo cha usalma walinzi wa pwani ya Italy ambao walituma mashua ya MSF Dignity 1 kuwaokoa.
Wakati mashua hiyo iliporudi kutia nanga ilikua imebeba wahamiaji 316 kutoka maeneo tofauti ya usaidizi katika bahari ya shamu.
Christine
Christiana alikua miongoni mwa wanawake 36 kwenye mashua hiyo. Kulikua pia na watoto 4 mdogo Zaidi akiwa na umri wa miezi mitatu. Walisimulia jinsi wengine wao walivyopigwa, kutekwa nyara, kubakwa na hata kufungwa jela wakiwa Libya.
Walipowasili katika eneo la Vibo Valentia, katika pwani ya Kusini magharibi mwa Calabria nchini Italy, alisajiliwa na kutumwa hospitalini kufanyiwa ukaguzi wa kiafya .
Wanawake wengine wanne walijiunga naye ili kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya HIV kwa kuwa walibakwa huko Libya.
Christine
Baada ya muda wa masaa mawili alirudi na habari njema kuwa hali ya mtoto wake ilikuwa shwari. Ni mtoto wa kike na atapewa jina la mashua iliyo waokoa
Alipanda basi iliyokuwa ikielekea kusini mshariki mwa Italy akisubiri kuzaliwa kwa mwanawe Dignity.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)