Pages

Repost: Wakazi wa Dar es salaam Kupata matibabu yatakayotolewa na wataalamu kutoka Hospitali za Apollo

Ndugu msomaji, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, huduma ya kliniki na matibabu iliyotarajiwa kutolewa na Dkt. Alok Ranjan wa Hospitali za Apollo kutoka Hyderabad kwa kushirikiana na Hospitali ya Hindu Mandal tarehe 27Julai na 28Julai Mwaka 2015 imeahirishwa mpaka tutakapowatangazia tena.

Tunaomba radhi kwa usumbufu ambao unaweza kujitokeza.
Wakazi wa Dar es salaam Kupata matibabu yatakayotolewa na wataalamu kutoka Hospitali za Apollo.

Watanzania wanashauriwa kuitumia fursa hii ya kipekee ya ziara ya kitabibu itakayofanywa na madaktari kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad.  Kwa miaka mingi, watanzania wameshindwa kupata matibabu sahihi nchini kitendo ambacho kimewasababishia kusafiri nje ya nchi kupata matibabu sahihi ya mfumo wa fahamu, uti wa mgongo, figo pamoja na magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo.  Nia na madhumuni ya ziara ya madaktari na washauri hawa kutoka Hospitali za Apollo nchini Tanzania ni kuhakikisha kwamba wagonjwa wanapata vipimo sahihi kwa gharama nafuu. Madaktari bingwa watatu wanao ongoza katika Hospitali za Apollo watafanya kazi kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Hindu Mandal kutoa huduma za kimataifa kwa watanzania.

Wagonjwa wanaougua magonjwa yanayohusiana na uti wa mgongo, mishipa ya fahamu, figo na magonjwa ya kibofu cha mkojo, wanashauriwa kuhudhuria na kushiriki tukio hili la kipekee. Madaktari watatembelea wagonjwa, kufuatilia historia za wagonjwa na kuwashauri matibabu sahihi kutokana na ripoti za matibabu na vipimo.

Daktari wa kwanza atakayeshiriki katika kutoa ushauri na matibabu ni Dkt. Alok Ranjan ambaye ni mtaalamu katika upasuaji mishipa ya fahamu na uti wa mgongo katika Hospitali za Apollo mjini Hyderabad.  Atapatikana siku ya Jumatatu ya tarehe 27 Julai na tarehe 28 Julai kati ya saa 03 asubuhi  na 11 jioni kwa tarehe hizo mbili katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam.  Dkt. Alon Ranjan ni mtaalamu anayeongoza katika upausaji wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kwa zaidi ya miaka 20 kwa kufanya upasuaji mgumu wa mishipa. Dkt. Alok Ranjan ameongoza timu yake kufanya  pasuaji mbali mbali za mishipa ya fahamu zaidi ya 1,000  kama vile upasuaji mdogo wa mtindio wa ubongo, upasuaji wenye madhara madogo wa uti wa mgongo, upasuaji mgumu wa uti wa mgongo, na upasuaji kwa kutumia kifaa maalumu cha kuangalia uti wa mgongo na ubongo.  
Kliniki ya ushauri na tiba ya pili imepangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 31 Julai na 01 Agosti katika Hospitali ya Hindu Mandal ya Dar es salaam. Wagonjwa watapata fursa ya kupata ushauri na tiba kutoka kwa Dkt. Rajagopal ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa uzazi na Dkt. Sanjay Maitra ambaye ni mtaalamu wa figo kati ya saa 3 asubuhi na saa 11 Jioni kwa siku za Ijumaa na Jumamosi. Huduma hizi za ushauri na tiba, zitatolewa kwa gharama nafuu.

Dkt. Rajagopal  amebobea katika magonjwa ya mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi kwa wanaume. Amekuwa mshauri mwandamizi wa tiba wa magonjwa ya vina vya uzazi katika Hospitali za Apollo mjini Hyderabad tangu mwaka 1994.

Dkt Sanjay Maitra amebobea katika huduma na tiba za magonjwa ya figo na magonjwa yanayo shabihiana na haya.  Kwa kawaida madaktari hawa hutibu magonjwa sugu ya figo, uvimbe katika figo, figo zilizoshindwa kufanya kazi na jiwe figo ikiwa ni pamoja na kuelimisha juu ya masuala mbali mbali ya upandikizaji wa figo na usafishaji.  Dkt. Sanjay Maitra ana uzoefu wa miaka mingi katika tiba ya figo na alimaliza masomo yake ya utaalamu wa magonjwa ya figo kutoka katika chuo cha AIIMS mjini New Delhi. Dkt Sanjay Maitra pia amekuwa akitoa mafunzo ya upandikizaji wa figo kutoka katika miili iliyo kufa na iliyo hai, huduma muhimu za ubadilishaji wa figo, usimamizi wa mda mrefu wa usafishaji wa figo kwa wagonjwa.

Hii siyo mara ya kwanza kwa madaktari hawa kutembelea Dar es salaam.  Ushirikiano huu endelevu na Hospitali ya Hindu Mandal unathibitisha dhamira ya Hospitali za Apollo katika kutoa huduma bora za afya na nia thabiti ya kuendeleza mahusiano na Tanzania ambayo yameazishwa kwa Zaidi ya muongo mmoja.

Katika siku hizi ambazo madaktari hawa watatoa tiba na ushauri,  Dkt. Alok Ranjan, Dkt. Sanjay Maitra na Dkt. Rajagopal watakuwa wanapitia kujua hali za wagonjwa ambao waliwahi kutibiwa mjini Hyderabad au ambao walitibiwa kipindi ambacho madaktari hawa walitembelea Dar es salaam mara ya mwisho.  Katika kipindi hiki, madaktari hawa watafanya mahojiano na wagonjwa kujua historia ya ugonjwa wao, kuwafanyia vipimo, kujadili sababu zinazoweza kuwa vyanzo vya ugonjwa wao, matibabu yanayoweza kutolewa inchini, kuwaandikia wagonjwa dawa na kufanya mipango ya vipimo au kupendekeza matibabu ya ziada.  Kwa baadhi ya wagonjwa, kutegemeana na ukubwa wa tatizo la mgonjwa na hali yake, wagonjwa wanaweza kushauriwa kutafuta matibabu zaidi nje ya nchi kwa matibabu ambayo hayawezi kufanyika nchini Tanzania.  Katika kipindi hiki, wagonjwa watajadiliana na madaktari majibu ya vipimo au ripoti za vipimo vilivyofanyika hivi karibuni.  Kliniki hii ni fursa ya kipekee kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa yahusianayo na uti wa mgongo, mishipa ya fahamu, figo na magonjwa ya kibofu cha mkojo na ambao wanahitaji ushauri mbadala au wale ambao hawawezi kumudu gharama za kupata matibabu nje ya nchi.
Ndugu Radhey Mohan, Makamu wa Raisi wa Maendeleo ya Kimataifa Kibiashara anadhamini kliniki hizi kwa kushirikiana na Hospitali ya Hindu Mandal.

Wagonjwa wanahamasishwa kufaidika na kufursa hii na wanashauriwa kujiandikisha kupata ahadi ya  kuwaona madaktari hawa katika Hospitali ya Hindu Mandal kwa kupiga simu nambari +255 22 211 4991-4


Kuhusu Apollo
Mnamo mwaka 1983, Dkt. Prathap C Reddy, mbunifu wa afya nchini India, alianzisha hospitali ya kwanza ya ushirika nchini India, Apollo Hospitals Chennai. Kwa miaka mingi, Hospitali za Apollo zimeweza kukuwa kufikia kuwa moja ya shirika kubwa la afya barani Asia likiwa na uwezo wa zaidi ya vitanda 8,500 ndani ya Hospitali 50, zaidi ya maduka 1350 ya dawa na zaidi ya  kliniki za uchunguzi 100.  Pia Hospitali za Apollo  hutoa huduma za matibabu kwa utaratibu  wa kibiashara, huduma za bima za afya na kitengo cha tafiti za kitabibu kwa lengo la kufanya tafiti za magonjwa ya milipuko, seli shina za mwili na maumbile.  Kuendeleza vipaji ili kumudu hitaji linaloongezeka katika  utoaji wa huduma za hali ya juu, Hospitali za Apollo zina jumla ya vyuo 11 vya madaktari pamoja na wauguzi. Mafanikio haya yamezifaidisha Hospitali za Apollo kupata tuzo mbali mbali, ikiwa ni pamoja na tuzo ya kituo bora iliyotolewa na serikali ya India pamoja na kutambulika na tume ya pamoja ya kimataifa (Hospitali saba za Apollo zinatambuliwa na kutunukiwa na tume ya pamoja ya kimataifa). Katika heshima nadra, serikali ya India ilitoa mhuli wa kumbukumbu wa kuutambua mchango wa Hospitali za Apollo, ikiwa ni shirika la kwanza la afya kupata heshima hiyo.  Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo Dkt. Prathap C Reddy, alitunukiwa tuzo ya heshima ya ‘Padma Vibhushan’ mnamo mwaka 2010. Ushirika wa Hospitali za Apollo kwa zaidi ya miaka 50, umeendelea kuboresha uongozi katika uvumbuzi wa kitabibu, huduma za kliniki za kimataifa na maendeleo ya teknologia.  Hospitali zetu zimekuwa katika nafasi ya juu kimataifa katika huduma za kitabibu pamoja na utafiti. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)