Pages

News Alert: Lowasa Ajiunga Rasmi na Chadema, Asema anachukizwa na Umaskini na ndio maana marafiki zake ni matajiri

 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli kupitia CCM Mh Edward Lowasa akiingia katika ukumbi uliopo katika hoteli ya Bahari Beach Nje kidogo ya Jijini Dar tayari kwa kuongea na waandishi wa habari ambao ametangaza rasmi kuahamia chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
 Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano huo 

Mh Lowasa ajiunga Rasmi Ukawa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kutangaza kuwa ameamua kutafuta mabadiliko nje ya ccm mara baada ya kuona hajatendewa haki na CCM na kusema kuwa CCM aliyoiona Dodoma sio kama ccm iliyomlea huko nyuma.

Akiyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari Katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar Es Salaam Mh Lowasa aliendelea kusema kuwa "CCM sio mama yangu wala baba yangu" nakuirudia kauli hiyo mara mbili.

Mara baada ya Kuwatangazia waandishi wa habari katika mkutano huo vilevile Mkewe Mama Regina Lowasa alipokea kadi ya uanachama wa Chadema huku Mumewe Mh Lowasa akikabidhiwa kadi hiyo Na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Lowassa na mkewe wamekabidhiwa kadi zao za uanchama hii leo mbele ya viongozi wa vyama vya upinzani vya CUF,NLD na NCCR Mageuzi na matangazo hayo yanaoneshwa moja kwa moja na Azam TV pamoja na ITV. 


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)