Pages

News Alert: John Pombe Magufuli ndie atakayeipeperusha Bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao

Dkt John Pombe Magufuli

Hatimaye kile kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu na watanzania wengi hususani wanachama na wapenzi wa CCM kusikia kutoka Mkoani Dodoma katika Makao Makuu ya CCM Ni Kwamba John Pombe Magufuri ndie atakayeipeperusha Bendera ya ccm katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Octoba 25 2015.

John Pombe Magufuri ameshinda kwa kishindo kwa kupata  Asilimia 87 za kura huku akiwaacha mbali wapinzani wake Ambao Dkt Migiro amepata asilimia 10 ya Kura huku Dkt Amina Alli akishika Mkia kwa kupata Kura kwa asilimia 3.

Kwa Matokeo hayo yaliyotangazwa katika akaunti ya CCM kupitia mtandao wa twitter unathibitisha Matokeo hayo na kumfanya Dkt Magufuli kuwa Mpeperusha bendera kwa tiketi ya CCM.


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)