Pages

Man United imesajili Bastian Schweinsteiger

Man United imesajili Bastian Schweinsteiger
Manchester United imekubaliana na Bayern Munich kumsajili kiungo cha kati wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa ameieleza klabu yake kuwa hakutaka mkataba mpya ambao ungemuongezea muda baada ya mkataba ulioko sasa kukamilika ifikapo mwisho wa mwaka ujao.
Hata hivyo mkurugenzi mkuu mtendaji wa klabu hicho Karl-Heinz Rummenigge amekiri kuwa tayari Manchester United wamewasiliana nao.
''mwenzangu wa klabu ya man united amewasiliana na nami na tayari tumekubaliana nao'' alisema Rummenigge.
Schweinsteiger amecheza mechi 536 tangu ajiunge na klabu hiyo ya Bayern mwaka wa 2002.
Rummenigge "kwa hakika inahuzunisha sana kwani Bastian alikuwa ni kigogo wa timu hii.''
null
Schweinsteiger amekuwa Bayern Munich kwa miaka 17
"ametufanyia mambo mengi mazuri tu kwa hivyo alipoomba ruhusa ya kuondoka hatukuwa na budi''
''Kwetu ni heshima kwani ametuhudumia kwa miaka 17 kwa hivyo tukamuacha aendee akastaafie Uingereza'' alisema Rummenigge
Kusajiliwa kwake kunafikisha 3 idadi ya wachezaji waliosajiliwa baada ya mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos, na Muitaliano Matteo Darmian.
Yamkini Kocha Louis Van Gaal anatarajia kuzuru Marekani akiwa na kikosi dhabiti kwa mazoezi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)