Pages

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA 10 YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA VYUO VYA ELIMU YA JUU NCHINI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua  rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.  Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mvumbuzi wa mashine ya kuchujia maji safi, Dkt. Askwar Hilonga, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, Atilio Raphael (kushoto kwake) na William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani waliyoibuni maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani iliyobuniwa maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati  Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akioneshwa Plastiki zilizotengenezwa  kwa kutumia Mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo cha The United African University Of
Tanzania (UAUT) Chang Kilee, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo hicho katika Maonesho ya 10 ya
  Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya Mashine ya 3D Printer iliyobuniwa nchini Korea na inayotumika kufundishia wanafunzi wa IT wa Chuo cha 'The United African University Of Tanzania' (UAUT), wakati alipotembelea banda la maonesho la Chuo hicho katika Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Chuo hicho, Chang Kilee, akimpa maelezo kuhusu Mashine hiyo. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja kati ya mashine za kufanya miamala za Max Malipo, huku akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Machungu Msama,  wakati alipotembelea banda lao la maonesho katika Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini
yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tunguu Zanzibar, Hadi Mohamed  (kushoto) na baadhi ya wanafunzi wake, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo hicho kwenye Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya walimu, viongozi na wanafunzi wa Vyuo Vikuu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya walimu, Kung Fu na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udom.
 Dkt. Bilal, akisalimiana na mmoja wa Walimu wa Chuo cha Liaoning Shi hua, Liju Shi, wakati alipotembelea katika Banda lao.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, wakitoa burudani ya mchezo wa Kung Fu, wakati wa ufunguzi huo.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, wakitoa burudani ya mchezo wa Kung Fu, wakati wa ufunguzi huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)