Pages

LOWASSA ARUDISHA FOMU LEO MJINI DODOMA, ATEMA CHECHE KWA WANAOMTUHUMU




WAZIRI Mkuu Mstafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.


 Mh. Lowassa ambaye alikuwa amesindikizwa na Wenyeviti wa CCM wa mikoa 12 kutoka bara na visiwani, aliwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma majira ya saa 8:30 mchana wa leo Julai 1, 2015, na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Rajabu Luhavi. 


Baada ya kukabidhi fomu hizo, Mh. Lowassa, alikutana na waandishi wa habari na kusoma taarifa yake fupi, ambapo alionya wale wote wanaoeneza habari potofu kuwa yeye ni mla rusha, watoe ushahidi, wapi amekula rushwa, na ni  kiasi gani, za nani na wapi, Awataka Watanzania kupuuza habari hizo na kwani yeye ni muadilifu na hana shaka na hilo. Alisema, yeye ana fedha kiasi gani za kuwapa Wana CCM 874,297, waliojitokeza kumdhamini.


 "Maneno hayo sasa basi, natoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi huo autoe hadharani vinginevyo waache kueneza uvumi na uongo" Alisema Mh. Lowassa.  Alisema yeye anachukia umasikini, na kwamba endapo chama kitamteua na hatimaye Watanzania kumchagua kuwa Rais wa awamu ya Tano, atahakikisha anatimiza dhamira yake ya kuwaondolea Watanzania umasikini.




 Mh. Lowassa, ambaye alisindikizwa na Vigogo wa chama hicho akiwemo, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, na Mzee Pankrans Ndejembi wakiwemo wenyeviti wa CCM 12 kutoka Tanzania Bara na Visiwani, amehitimisha zoezi hilo baada ya kuzunguka mikoa 31 ya Tanzania Bara na Visiwani, na mara zote amekuwa akipata idadi kubwa ya wana CCM na wananchi waliojitokeza kwenye ofisi za CCM mahala alikopita, ikiwa ni pamoja na wengine kujipanga barabarani na kumpungia mikono

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati) akizipanga vyema fomu zake ili azikabidhi kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi (kushoto), wakati alipofika kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015. Mh. Lowassa amerudisha fomu hizo, baada ya ziara yake ya nchi nzima kutafuta saini za WanaCCM wa kumdhamini ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015, ambapo jumla ya WanaCCM 874,297 walimdhamini.Kushoto kwa Mh. Lowassa ni Mkewe, Mama Regina Lowassa.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi fomu za wanaCCM waliomdhamini ili aweze kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi wakionyesha fomu hizo kwa wanahabari wakati wakikabidhiana, kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kurudisha fomu za wanaCCM waliomdhamini ili apare baada ya ziara yake ya nchi nzima kutafuta saini za WanaCCM wa kumdhamini ili aweze kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)