Mahusiano kati ya Tanzania na India
yalianza miaka mingi iliyopita, tangu kipindi hicho mahusiano haya yamekua
kufikia mafanikio ya hali ya juu kwa nchi zote mbili. Rais Jakaya Kikwete alitembelea nchini India
ambapo alikutana na maafisa mbali mbali wa Serikali hiyo ya India pamoja na
maafisa watendaji wakuu wa makampuni pamoja na
taasisi mbali mbali. Pia wakati
wa ziara hii Rais alisaini makubaliano ya kushirikiana kati ya serikali ya
Tanzania na Hospitali za Apollo nchini India.
Wakati wa ziara hii ya kitaifa Rais
Jakaya Kikwete nchini India iliyofanyika tarehe 17 hadi 21 June 2015, Rais
aliambatana na ujumbe wa ngazi za juu ikiwa ni pamoja na mawaziri na maafisa
waandamizi wa India. Rais alifanya
mazungumzo ya kina na Waziri Mkuu wa India Bwana Narendra Modi ambapo Rais
aliishukuru India kwa misaada endelevu kwa Tanzania na kusema kuwa nchi zote
zimeamua kuendeleza mahusiano zaidi.
Kihistoria Tanzania na India zimeendelea
kufurahia mahusiano ya kirafiki yaliyojikita katika kufaidisha pande zote
kibiashara na mawasiliano baina ya watu na watu. India ni mdau mkubwa wa biashara Tanzania
ambapo biashara baina ya nchi hizi mbili mnamo 2013-14 umekuwa wa zaidi ya dola
za Kimarekani bilioni 4. Mbali na mahusiano haya ya kibiashara, India pia ni
kimbilio la watanzania wanao tafuta
huduma za kiafya za hali ya juu pamoja na elimu.
Umoja wa Hospitali za Apollo una
hazina kubwa ya ushirikiano na watu wa Tanzania. Hospitali zimetoa matibabu kwa watanzania kwa
miaka kadhaa. Madaktari bingwa wa
Hospitali za Apollo wamekuwa wakitembelea Tanzania mara kwa mara kwa ajili ya
kutoa ujuzi wao wa kimatibabu kwa wagonjwa wa ndani ya nchi. Madaktari bingwa wa Apollo pia wametoa
mafunzo kwa madaktari wa Tanzania pamoja na wauguzi miaka michache iliyopita.
Hii imewawezesha wafanyakazi wa hapa nchini kuchukua nafasi za kiufundi, muhimu
na za usimamizi katika jamii.
Rais alitembelea wagonjwa waliolazwa
katika Hospitali za Apollo ambapo alipata nafasi ya kuonana na madaktari bingwa
pia kuonana na familia za wagonjwa waliolazwa katika Hospital hiyo. Rais
alipewa taarifa ya hali za wagonjwa na maendeleo ya matibabu wanayoendelea
kupatiwa. Kutokana na uhaba wa huduma
bora za kimatibabu kwa gharama nafuu, watanzania wengi wanalazimika kusafiri
nje ya nchi kwa matibabu. Hii huwasababishia wagonjwa kupata matibabu ya kina
wakiwa mbali na msaada wa familia, ndugu na marafiki.
Wakati wa ziara yake Mheshimiwa
Jakaya Kikwete alisaini mkataba wa mahusiano na Hospitali za Apollo na shirika
la mfuko wa jamii la Tanzania NSSF.
Kliniki itaanzishwa miezi michache ikifuatiwa na Hospital nchini
Tanzania. Hii itawasaidia watanzania kupata huduma ndani ya nchi itakayo
wawezesha wananchi kupata huduma maalumu pasipo kutumia gharama kubwa ya
kusafiri nje ya nchi. Hii pia itasaidia
kuboresha huduma za kiafya kwa kutoa mafunzo zaidi kwa wataalamu wa afya wa
ndani ya nchi.
Kuhusu
Apollo
Mnamo mwaka 1983, Dkt. Prathap C
Reddy, mbunifu wa afya nchini India, alianzisha hospitali ya kwanza ya ushirika
nchini India, Apollo Hospitals Chennai. Kwa miaka mingi, Hospitali za Apollo zimeweza
kukuwa kufikia kuwa moja ya shirika kubwa la afya barani Asia likiwa na uwezo
wa zaidi ya vitanda 8,500 ndani ya Hospitali 50, zaidi ya maduka 1350 ya dawa
na zaidi ya kliniki za uchunguzi
100. Pia Hospitali za Apollo hutoa huduma za matibabu kwa utaratibu wa kibiashara, huduma za bima za afya na
kitengo cha tafiti za kitabibu kwa lengo la kufanya tafiti za magonjwa ya
milipuko, seli shina za mwili na maumbile.
Kuendeleza vipaji ili kumudu hitaji linaloongezeka katika utoaji wa huduma za hali ya juu, Hospitali za
Apollo zina jumla ya vyuo 11 vya madaktari pamoja na wauguzi. Mafanikio haya
yamezifaidisha Hospitali za Apollo kupata tuzo mbali mbali, ikiwa ni pamoja na
tuzo ya kituo bora iliyotolewa na serikali ya India pamoja na kutambulika na
tume ya pamoja ya kimataifa (Hospitali saba za Apollo zinatambuliwa na
kutunukiwa na tume ya pamoja ya kimataifa). Katika heshima nadra, serikali ya
India ilitoa mhuli wa kumbukumbu wa kuutambua mchango wa Hospitali za Apollo,
ikiwa ni shirika la kwanza la afya kupata heshima hiyo. Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo Dkt.
Prathap C Reddy, alitunukiwa tuzo ya heshima ya ‘Padma Vibhushan’ mnamo mwaka
2010. Ushirika wa Hospitali za Apollo kwa zaidi ya miaka 50, umeendelea
kuboresha uongozi katika uvumbuzi wa kitabibu, huduma za kliniki za kimataifa
na maendeleo ya teknologia. Hospitali
zetu zimekuwa katika nafasi ya juu kimataifa katika huduma za kitabibu pamoja
na utafiti.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)