Pages

CHADEMA YAANDAA KONGAMANO LA WAZEE, KUFANYIKA KESHO HOTELI YA BLUE PEARL UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Hashim Juma Issa (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu kongamano litakalo wakutanisha wazee wote bila kujali itikadi za vyama vyao litakalo jadili mustakabali wa taifa kuelekea uchaguzi mkuu litakalofanyika  kesho ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Makamu  Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Suzan Lymo, akizungumza katika mkutano huo.
 Baadhi ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeandaa  kongamano la wazee ambalo litafanyika Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam kesho.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo mchana  Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la chama hicho, Hashim Juma Issa alisema kongamano hilo litawahusisha wazee wote nchini bila ya kujali itikadi za vyama vyao.

Alisema dhima kubwa ya kuanzisha kongamano hilo ni kuwapa elimu wazee bila kujali itikadi zao za kisiasa  hasa katika kipindi hiki cha  kuelekea uchaguzi mkuu. 

"Wazee wengi wamekuwa hawafahamu nini majukumu yao kama wazee lakini kongamano hili litakuwa ndiyo chanzo kikubwa cha 
kuwafahamisha wazee majukumu yao hasa katika wakati huu wa 
kuelekea uchaguzi," alisema Issa.

Alisema kila mtu anafahamu  binadamu huwa anapitia hatua muhimu za maisha nazo ni utoto,ujana na utu uzima hivyo hamna budi wazee hawa kuelewa lengo kuu katika katika uchaguzi mkuu huo kuwa katika mstari ulinyooka. 

"Kumekuwa na tabia ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwatumia wazee kwa ujanja tena hasa wakiwa na matatizo na kuwabagua wa vyama vingine lakini sisi katika kongamano hili hatutobagua mzee wa chama chochote katika kongamano hili kwani wazee wote ni hazina,"alisema

"Hakuna asiyefahamu kuwa kwa sasa nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu ambao uchaguzi huu utakuwa ni mkubwa na wa aina yake hivyo kwa kuwaita wazee hawa itakuwa ni muendelezo wa kupata hekima zao kama wazee"alisema.

Issa alisema katika uchaguzi mku wazee wana jukumu kubwa la 
kuhakikisha kushiriki kikamilfu katika zoezi zima la kujiandikisha na kupiga kura ipasavyo.

Alisema hatua hiyo haina budi kuwasahawisi watoto na watu wakubwa na wajukuu kushiriki kwa ukamailifu katika tukio hili kwani kila mtu anahitaji mabadiliko katika nchi.

Hata hivyo Issa alisema wazee pia wana jukumu kubwa la kutatua 
migogoro ,kushawisi na kusimamia maadili lengo likiwa ni uthubutu wa kukemea viongozi wanaopata madaraka kwa njia ya rushwa na ufisadi.

Alisema wanahitaji wazee watakaosimama kidete na kupaza sauti zao katika kukemea maovu na watenda maovu bila kuona haya.

Alisema katika kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Wilbroad Slaa huku mada mbalimbali zitatolewa na Mabere Marando pamoja na viongozi wa dini ili kuwapa elimu wazee kutokana na maadili ya nchi kumomonyoka kwa kiasi kikubwa. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)