Pages

ACACIA YATANGAZA UDHAMINI MNONO KWA STAND UNITED YA SHINYANGA, NI WA MIAKA MIWILI

 MENEJA Mkuu wa kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, Asa Mwaipopo, (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandihi wa habari makao makuu ya kampouni hiyo barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, leo Julai 8, 2015. Kampuni ya Acacia, inayomiliki migodi ya kuchimba dhahabu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, imetangaza udhamini wa miaka miwili itakayotoa kwa klabnu ya soka ya Stand United ya mkoani Shinyanga. Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu iko mkoani humo. Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United ya Shinyanga, Amani Vincent, na kushoto ni Meneja wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia mahusiano ya kijamii, Stephene Kisakye
Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United ya Shinyanga, Amani Vincent akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Julai 8, 2015 kuhusu kuingia mkataba wa udhamini wa klabu hiyo na kampuni ya uchimbaji madini, Acacia.Udhamini huo utakuwa wa miaka miwili, kwa mujibu wa Meneja Mkuu anayeshughulikia uendelezaji wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo.(katikati). Kushoto ni Meneja anayeshughulikia mahusiano ya kijamii wa kampuni ya Acacia, Stephen Kisakye.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)