Pages

Wadau: Filamu ya Mpango Mbaya ina viwango vya Kimataifa

Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group, Bw Johnson Lukaza akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa filamu ya Mpango Mbaya iliyochezwa na washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) mwaka 2014, uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa sinema wa century uliopo Mlimani City, Jijini Dar Es Salaam. Filamu hii ni moja ya filamu ambayo ina ubora wa hali ya juu huku wadau waliofanikiwa kuitazama filamu hiyo kuvutiwa nayo na kukubali kuwa ni filamu yenye viwango vya kimataifa na yenye utofauti mkubwa na filamu nyingine za Kitanzania.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group, Bw Johnson Lukaza akifurahia jambo na mwenyekiti wa bodi ya filamu nchini, Mama Fisoo kabla ya uzinduzi wa filamu ya Mpango Mbaya kuanza, uzinduzi huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa Sinema wa Century uliopo Mlimani city, Jijini Dar Es Salaam
Muongozaji wa filamu ya Mpango Mbaya, Kalabani Kalabani akizungumzia juu ya filamu ya mpango mbaya aliyoiongoza
 Mmoja wa washiriki katika filamu hiyo Anneth Peter (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa host wa TMT 2015 Mboto Haji (katikati) na Mwalimu wa washiriki wa filamu Hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Mwl Issa
 Mshiriki wa filamu ya Mpango Mbaya Said (kulia) akijiachia mbele ya kamera ya Lukaza Blog kabla ya uzinduzi wa filamu ya Mpango Mbaya uliofanyika Mlimani City
Muongozaji wa Filamu ya Mpango Mbaya, Kalabani Kalabani (katikati) akijadiliana jambo na mmoja wa Washiriki wa filamu hiyo ambae ndie aliyekuwa mwigizaji msaidizi katika filamu ya Mpango Mbaya Mzee Adolph

Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)