Pages

Vuna mbegu za kiume mkiwa na miaka18

Mbegu za uzazi wa wanaume zinapaswa kuvunwa na kuhifadhiwa pindi mtu anapotimiza umri wa miaka 18.
Mbegu za uzazi wa wanaume zinapaswa kuvunwa na kuhifadhiwa pindi mtu anapotimiza umri wa miaka 18.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtafiti wa maswala ya uzazi nchini Uingereza, manii ya mwanaume huwa katika hali bora zaidi wakati huo na hivyo zinapaswa kuvunwa na kisha kutumika kupandikiza wanawake katika siku za usoni.
Daktari Kevin Smith, ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Abertay kilichoko Dundee Uingereza anasema kuwa baada ya utafiti wa kipindi kirefu amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ilikuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.
null
Dakta Kevin Smith, anasema kuwa wizara ya afya ya Uingereza inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi
Daktari Kevin Smith ameorodhesha ugonjwa wa akili ''autism'', na ule wa kuchanganyikiwa ama ''schizophrenia'' miongoni mwa magonjwa mengine mengi.
Dakta Smith, anasema kuwa wizara ya afya ya Uingereza inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi ilikupunguza visa vya maradhi aliyoorodhesha.
Maoni yake hata hivyo yanapingwa na muungano wa wauguzi wa uzazi ambao wanasema kuwa hilo halitakuwa suluhisho la kudumu.
Badala yake shirika hilo linaitaka serikali ya Uingereza iweke sera zitakazowasaidia waingereza waliofikia umri wa uzazi kupata ajira.
null
Manii yakivunwa mapema yatasaidia kuepuka maradhi mengi tu
Takwimu zinaonesha kuwa wanaume wanaanza kupata watoto wakiwa na umri wa miaka 33 ikiwa ni ongezeko kutoka kwa miaka 31 katika miaka ya tisini.
Akitetea wazo lake katika jarida la madaktari la ''The Journal of Medical Ethics, Dakta Smith nasema kuwa wale wanaotaka kupata watoto mapema basi wafanye hivyo lakini kwa wale ambao wamegonga maiaka 40 ni vyema watumie mbegu walizohifadhi kwa matokeo mazuri zaidi.
Profesa Adam Balen, wa shirika la British Fertility Society, ameonya kuwa mbegu ziliyohifadhiwa huwa hazina nguvu kama zile zinazotolewa moja kwa moja.
null
Amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ilikuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.
''Kwa mtazamao hawa vijana wanahitahitaji ajira na wapenzi basi watapata watoto pasi na matatizp yeyote.''alisema Profesa Balen
Wakati huo huo mwanasayansi mwenza Sheena Lewis, aliwashauri wanaume waanze kushughulikia swala la familia mapema katika ujana wao.
''ninataka kuwaelezea wazi kuwa umri mzuri wa kuzaa kwa wanaume na wanawake ni kati ya miaka ya 20 na 30."

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)