Pages

Tangazo la Msiba wa Aliyekuwa Kamishna wa Magereza Onel Malisa

unnamedKamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara kuanzia Mwaka 1996 hadi 2002, Onel E. Malisa kilichotokea leo Alfajiri tarehe 2 Juni, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dares Salaam.
Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu linaendelea kuratibu taratibu zote za kuaga na mazishi ya marehemu. Hivi sasa msiba upo nyumbani kwake Kinyerezi, Jijini Dar es Saalam. Aidha taarifa kamili kuhusiana na msiba huu mtaendelea kufahamishwa baada ya mipango yote kukamilika.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi;
AMINA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)