Pages

Swali letu la Msingi: Kauli hii unaichukuliaje "Nipe Mia Nikupe Mia Mbili" ndani ya daladala

Leo katika swali letu la msingi tutaongelea swala la makondakta wengi kuchukulia swala la "nipe mia nikupe mia mbili" kipindi unapotoa nauli na unatakiwa kurudishiwa shilingi Mia.

Picha Kwa Hisani ya Mtandao
Kauli hii imekuwa maarufu sana na imekuwa kama sheria katika usafiri wa umma yaani daladala na pindi utoapo Shilingi Mia tano kulipa nauli ambayo ni shilingi Mia 4 lazima utakuwa umeshakutana au kusikia kauli hii.

Hali hii nimekuwa nikiishuhudia mara kwa mara pindi nipandapo daladala na wakati mwingine nimekuwa nikisikia baadhi ya abiria wakiwatolea sauti ya juu makondakta pindi wanapowauliza kuwa "Una mia nikupe Mia Mbili" kwangu mimi naichukulia kauli hii kama ni sehemu tu ya urahisishaji wa upatikanaji wa cheji hususani Shilingi Mia mia maana shilingi mia imekuwa kazi kuipata kwenye daladala sababu kwanini hazipatikani sana naweza sema ni kutoka na pesa nyingi zinazotumika katika mzungo ni za noti na nauli unakuta ni Mia 4 sasa ukitoa mia tano lazima urudishiwe mia na ndio hapo konda atakuuliza "Una Mia nikupe Mia Mbili"

Kama na wewe ni mpandaji wa daladala utakuwa ushakutana na kauli hii je naomba kuuliza usikiapo kauli hii kutoka kwa konda unaichukuliaje na unawachukuliaje abiria wanaowatolea lugha ya kejeli na juu pindi konda akiwauliza swali hilo.

Tuajdiliane hapa kwa kutoa mawazo yako sehemu ya komenti na sisi tutayaachia bila kuweka jina lako kama hutopenda.

Kusoma Maswali ya msingi yaliyotangulia unaweza kuyasoma kwa KUBOFYA Hapa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)