Pages

Simba kujadili mkataba wa Singano

Ramadhani Singano (kulia) akiwa na aliyekuwa mchezaji wa Simba, Amisi Tambwe, anayecheza Yanga kwa sasa
Uongozi wa klabu ya Simba umeagizwa kuanza mazungumzo mapya na mchezaji Ramadhani Singano (Messi) baada ya mvutano wa utata wa mkataba wake.
Messi na Simba waliingia katika utata wa usajili, baada ya mchezaji huyo kudai mkataba wake umeisha msimu huu, huku uongozi ukieleza kuwa bado anatakiwa aitumikie timu yake hadi msimu ujao.
Kwa mujibu wa Afisa mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, TFF imekutana na uongozi wa klabu ya Simba SC ukiwakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collin Frisch na mchezaji Ramadhani Yahya Singano aliandamana na uongozi wa Chama cha Wacheaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA) katika kutafuta suluhu ya jambo hilo.
Kizuguto alisema kikao hicho kiliitishwa na TFF ili kujadili na kutafuta ufumbuzi wa utata wa kimtakabta kati ya mchezaji na klabu ya Simba.
Amesema katika kikao cha leo (Jumanne) pande zote zimeeleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC.Amesema kuwa kwa pamoja, pande hizo mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya na hatimaye mkataba mpya utakaoanza katika msimu mpya wa 2015/16.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)