Pages

NEWS FLASH: MSAFARA WA MAKONGORO NYERERE WAPATA AJALI MBAYA MKOANI KIGOMA

Gari lililopata ajali katika msafara wa Mgombea urais, Charles Makongoro Nyerere lililokuwa limebeba wasaidizi wake.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya kasulu wakishangaa ajali ya gari la wasaidizi wa mgombea urais kupitia CCM, Charles Makongoro Nyerere.
Msafara wa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Makongoro Nyerere umepata ajali wilayani Kasulu mkoani Kigoma mapema leo hii.

Msafara huo uliokuwa ukielekea wilayani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini, ambapo gari walilokuwa wamepanda wasaidizi wa Makongoro ndilo lililopata ajali kwa kupinduka wakati likiwa kwenye mwendo.

Watu waliokuwepo katika gari hilo lililopata ajali wameumia vibaya sana akiwemo Mwandishi wa habari, Cyprian Musiba na kukimbizwa katika hospital ya wilaya ya kasulu (mlimani) kwaajili ya matibabu.

tutaendelea kuwajuza zaidi juu tukio hilo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)