Saudia
Mahakamu kuu nchini Saudia imeamua kuwa hukumu ya kifungo cha miaka 10 na viboko 1000 dhidi ya mwanablogu Raif Badawi aliyepatikana na hatia ya kutukana Uislamu itabaki vile ilivyo
Utalawa nchini Saudi Arabia uliamuru kusikilizwa tena kwa hukumu hiyo kufuatia shutuma za kimataifa baada ya bwana Badawi kuchapwa viboko hamsini mapema mwaka huu.
Mkewe na makundi ya haki za kibinadamu yameonya kuwa huenda akafariki ikiwa hukumu hiyo yote itatekelezwa.
Bwana Badawi alikamatwa kufuatia blogi aliyoanzisha ambayo ilikashifu baadhi ya tamaduni nchini Saudi Arabia.bbc
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)