Pages

MHE. ZITTO KABWE: JANUARY MAKAMBA ASHINDWA KUTAMKA MIIKO YA VIONGOZI

Mheshimiwa Zitto Kabwe amefunguka katika ukurasa wake wa Facebook na kuweza kumponda mbunge mwenzake wa Bumbuli, Mheshimiwa January Makamba kutokana na Hotuba yake aliyoisoma jana katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam wakati akitangaza nia ya Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania mwaka 2015.

Ujumbe akiyouandika Mheshimiwa Zitto Kabwe...

January Y. Makamba ndiye mgombea wa CCM aliyejieleza kwa ufasaha zaidi kuliko wote. 'content' kawazidi wenzake wote. Hata hivyo ameshindwa kabisa kutamka Miiko ya Viongozi. Bila Miiko yote aliyoyataja hayatafanyika maana ufisadi utatamalaki. Unaweza kuondoa rushwa kwa sheria. Lakini huwezi kuondoa ufisadi bila Miiko ya Viongozi. Sijui kwanini Kijana mwenzangu kaona aibu japo kutaja neno Miiko. Uchaguzi wa mwaka huu umeegemezwa kwenye kurudi kwenye Misingi iliyoasisi Taifa.

Nimeridhika sana na content na context. Sikubaliani na mwono. January Makamba anaiona Tanzania ya kibepari. Nadhani inabidi kufumua uchumi wa kibepari na kujenga uchumi wa kijamaa. I would love to debate him on the kind of the nation we shall rebuild. Kila la kheri rafiki yangu.

Maono ya watu waliyoyatoa....

Faraja MG.
Ubepari ndo wenyewe. Ujamaa tulishauzika. Huwezi endelea na Ujamaa.

Jimy Macha
Katumia sana shule kwenye kujieleza kuliko uhalisia.....

Joseph Pjp.
Ingekuwa tunawapima wagombea kwa kujieleza basi nchi hii ‪#‎MC‬ wa sherehe wangefaa kuwa marais wetu! na watunga hotuba kama yeye , hiyo ilikuwa ajira yake kuandika hotuba.

Kimsingi January ni uzao wa huo mfumo anaoulalamikia kuwa atauletea Mabadiliko! ‪#‎Baba‬ yake amekuwa kwenye same system ‪#‎iliyofeli‬ anayoilalamikia kuwa imefeli! for 50 years ‪#‎genetically‬ he has proved us right kuwa hana jipya sawa na wazazi wake walivyofeli na yeye amefeli! refer ‪#‎simcardTax‬ na tozo ghali za simu , MB 8 , hayo ni mambo madogo tuu kafeli.

hatujasahau hiyo sheria ya mitandao aliyekuja nayo ya kuzima moto na sasa haiwezi kufanya kazi. inshort ni ngumu fisii kuzaa swala!
sio mimi, ni kanuni ya Genetics!

David Mssika.
January Y. Makamba did well. Maybe hizo kasoro ziwe ni challenge kwake. Nimependa ufufuaji wa njia za uchumi na mikakati YA kuongeza/kupata fedha from within! Hii itapunguza dependency syndrome! Kitu nimekosa kwa wote Usalama wa raia na Mali zao, usalama wa nchi na namna YA kuboresha demokrasia.

Albert Kamwela.
Nina shaka na utekelezaji. Maneno yanakuwa mengi kuliko utekelezaji.

Goodluck Andrew Msaky.
Hivi mradi wa MKURABITA ungeenda ipasavyo hawa watia nia wangezungumza kitu gani? Anatuambia ataunda baraza la mawaziri18 lenye maadili wakati hiyo sera ilikuwepo kwenye rasimu ya katiba ya Jaji Warioba na ndiyo hiyo CCM wameipiga vita bungeni akiwemo sasa leo anatuambia kitu gani.. Naona kama anakosoa yaliyofanywa kipindi cha awamu ya nne na yeye alikua na uwezo wa kushauri kama naibu waziri mambo yakaenda sawa.

Manywele Omary.
Chui katika Ngozi ya kondoo.. Nadharia na Vitendo ndo tofauti kubwa kwa viongozi wa CCM, so far me naona Mwigulu Nchemba ndo yupo na real inner spirit ya mabadiliko.

Lyaruu Engelbert John.
Ni mkusanyiko wa yale yale!! Kweli hatujapata jibu la changamoto zetu. Hawa walikuwa na rais mbona haya wanayoongea hawakufanya katika wizara zao; au rais hakuwa na utashi! Tujiulize.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)