Pages

MFANYAKAZI WA GLOBAL, ROBERT TILLYA AAGWA JIJINI DAR, KUZIKWA KILIMANJARO

Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Lydia Bukumbi akiaga mwili wa Robert Tillya.
Mwandishi wa Global Publishers, Mayasa Mariwata akiuaga mwili wa mfanyakazi mwenzake kwa simanzi.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (wa kwanza kulia), Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka (wa tatu kulia) na Ofisa Utawala wa Global, Soud Kivea (wa pili kushoto) wakiwa na simanzi wakati wa zoezi la kuaga mwili wa Robert Tillya.
Elvan Stambuli akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Global Publishers Ltd.
Wafanyakazi wa Global wakiongozwa na Imelda Mtema (wa kwanza kushoto) kuaga mwili wa Robert.
Wafanyakazi wa Global, ndugu, jamaa na marafiki wakiuaga mwili wa Robert kwa simanzi nzito.
Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist akiaga mwili wa Robert kwa huzuni.
Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli akiaga mwili wa marehemu.
Mhariri wa Championi Jumatano, Phillip Nkini akiaga mwili wa Robert.
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Richard Manyota akiuweka vizuri mwili wa Robert tayari kwa zoezi la kuaga.
Mwili wa Robert Tillya ukipelekwa kwenye gari.
Waombolezaji wakijiandaa kuingia kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Kilimanjaro.

MWILI wa aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Robert Tillya hatimaye leo umeagwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa maziko.

Marehemu Tillya alikuwa dereva wa Global na alifikwa na mauti Jumamosi iliyopita alfajiri baada ya kupata ajali maeneo ya River Side, Ubungo jijini Dar.

Mamia ya waombolezaji wakiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, wafanyakazi wa Global, ndugu, jamaa na marafiki waliungana katika Hospitali ya Mwananyamala kumuaga mpendwa wao majira ya saa tano asubuhi.

Marehemu Tillya alizaliwa Novemba 18, 1981 na ameacha watoto wawili wa kiume na wa kike. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Tillya mahali pema peponi. AMEN.  (PICHA NA MUSA MATEJA / GPL)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)