Pages

MBUNGE WA GEITA, DONALD MAX KUZIKWA JUMAMOSI

Donald Kevin Max (58) enzi za uhai wake.
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini (CCM), Donald Kevin Max (58) anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi ya Juni 27, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Marehemu Max enzi za uhai wake akiwa na Beno Malisa (kulia).
Akitangaza taarifa za msiba huo, mapema leo asubuhi bungeni mjini Dodoma, Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko, ambapo mbunge huyo alifariki jana katika HospitalI ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa muda mrefu.
Spika Makinda amesema taarifa za awali zinasema mwili wa marehemu utazikwa siku ya Jumamosi jijini Dar lakini bado anaendelea kuwasiliana na familia ya marehemu.
Kufuatia msiba huo, Spika ameliahirisha bunge mpaka kesho saa 3 asubuhi.
Mungu ailaze roho ya marehemu, mahali pema peponi, AMEN.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)