Pages

MAONESHO YA UTALII YA SANGANAI/HLANGANANI–(WORLD TOURISM EXPO) ZIMBABWE YAFUMBUA MACHO WATANZANIA

IMG_4145
Pichani juu na chini ni Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kushoto) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vyake nchini Tanzania kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali vikiwemo vya utalii nchini Zimbabwe waliofika katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya nane ya Kimataifa ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) kupata taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii wa Tanzania yaliyomalizika jana jijini Harare katika ukumbi wa hoteli ya Rainbow Towers.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
IMG_4137

IMG_4168
Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) akibadilishana mawazo na wananfunzi wa Belvedere Technical Teachers College nchini Zimbabwe, Francisca Chipuriro (kushoto) na Natalie Takavarasha (katikati) wakati walipotembelea banda la Tanzania kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali za utalii wa Tanzania na vivutio vyake siku ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers.
IMG_4185
Wageni mbalimbali waliovutiwa na vivutio vya utalii nchini Tanzania wakiendelea kumiminika katika banda la Tanzania na kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) ambapo hivi sasa Shirika la ndege la Fastjet limeanza safari zake jijini Harare kupitia Lusaka hadi Dar es Salaam kwa gharama nafuu kabisa itakayowezesha wananchi wa Zimbabwe kufanya safari za Tanzania kwa gharama nafuu kabisa.
IMG_4229
Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii zinazofanywa na kampuni yake kwa wageni waliofika katika banda la Tanzania wakati wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare.
IMG_4241
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (wa pili kulia) akitoa maelezo yaliyomo kwenye vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii nchini Tanzania kwa wageni waliotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho nane ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.
IMG_4191
Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel ya nchini Tanzania, Joseph Waryoba (kulia) akipata picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini Zambia, Felix Chaila aliyembelea banda la Tanzania wakati wa maonesho ya siku tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers ambayo yamemalizika juzi.
IMG_4195
Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel nchini Tanzania, Joseph Waryoba katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tanzania Travel Company ambayo pia imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.
IMG_4205
Timu kutoka Tanzania ambayo imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare ikiongozwa na Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel nchini Tanzania, Joseph Waryoba, Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (kulia).

Na Modewjiblog team, Harare
TIMU ya watanzania walioenda kuhudhuria maonesho ya utalii nchini Zimbabwe wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza uendeshaji wa sekta ya utalii. Walisema katika ziara yao hiyo wamegundua kwamba Wazimbabwe kuanzia wanapompokea mgeni hadi anapofika hotelini wanaonesha kujali hali ambayo mgeni hawezi kusahau hata kidogo.

Aidha amesema kwamba hata mipangilio ya kwenda kwenye vivutio inafanyika katika hali ambayo huwezi kusahau hata kidogo. Kutokana na mazingira hayo, wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza namna ya kupokea na kuishi na wageni na kuwatengenezea taswira ambayo hawatakaa wakisahau.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog yaliyofanyika mjini Harare siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya siku tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers jijini Harare.

Solomon amesema ingawa hali ya Tanzania si mbaya, watendaji katika viwanja vya ndege na mahotelini wanaweza kuangalia namna Wazimbabwe wanavyojali kazi zao na tabasamu zao nyakati zote kwa wageni . “Si kwamba kwetu kuna shida lakini unaona watu wanavyojituma hapa” alisema Esther Solomon na kuongeza kuwa aliona jinsi walivyojipanga vizuri na wafanyakazi walikuwa na uelewa wa hali ya juu.

Esther aliongoza kundi la watu watano wa Kitanzania walioalikwa na mamlaka ya utalii Zimbabwe (ZTA) kuhudhuria maonesho hayo.Tanzania iliweka banda lake pia katika maonesho hayo ya siku tatu yaliyomalizika juzi. Makampuni ya mawakala wa utalii aliyoambatana nayo katika safari hiyo ni pamoja na Tanzania Travel Company, Cordial Tours and Travel, Mberesero Tented Camp na Best Northern Tours and safaris .

Alisema safari yao Zimbabwe pamoja na ushiriki wao katika maonesho pia walifika katika maeneo mbalimbali ya kitalii nchini yakiwemo maporomoko ya Victoria.
Aidha walipewa nafasi ya kukagua sehemu za malazi kwa ajili ya wageni.
Alisema katika maonesho hayo wamefanikiwa kupata wageni wengi wanaoulizia namna ya kufika Tanzania na pia ushirikiano wa makampuni katika sekta ya utalii.

“ Watu wengi wamekuja kututembelea. Na wengi ni watu weusi. Mwamko wao wa kutembelea vivutio ni mkubwa.” Alisema Esther na kuongeza kuwa wamebaini kwamba ipo haja ya watanzania kuhimizwa kutembelea vivutio kwani hata nchini Zimbabwe wanaotembelea vivutio ni wananchi wenyewe.

Alisema wengi waliofika katika banda la Tanzania waliulizia namna ya kufika visiwa vya Zanzibar na pia mbuga za Tanzania. Aidha mawakala wengi waliulizia namna ya kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha utalii katika bara la Afrika. Asilimia 80 ya watalii nchini Zimbabwe wanatoka bara la Afrika na waliobaki ndio wanatoka nje ya bara hili.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)