Pages

MABOMU YATAWALA CHUO CHA KAMPALA

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Kimataifa Cha Kampala (KIU) wakiwa katika maandamano leo katika chuo hicho baada ya Kitivo cha Famasia kushindwa kutambulika na mamlaka mbalimbali.
 Askari wa Polisi wakiwa katika gari na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) waliowakamata katika maandamano hayo.
Rais wa  Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIUPESO),Elias Mbogho akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maandamano yaliyofanyika leo katika hicho jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi,Jamal Mohamed.
 Wanafunzi wa KIU wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.
 Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa kazini  leo katika Chuo  Kikuu cha Kampala jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu  cha Kampala akiwa na majeraha katika maandano yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakiwa katika maandamano katika Chuo Kikuu  cha Kampala leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Cha Kampala (KIU) leo wameandamana na katika chuo hicho kushinikiza warudishe fedha zao kutokana na kuanzisha kitivo ambacho hakitambuliki na mamlaka za nchi.

Mgomo huo umeanza majira ya saa tatu kwa baadhi wanafunzi kuwazuia wenzao wasiingie katika chumba cha mtihani na baada ya hapo wakaibuka na mabango kwenda katika ofisi za utawala wa chuo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika chuo hicho,Rais wa Serikali wa Chuo Kikuu cha Kampala(Kiupeso),Elias Mbogho amesema kuwa maandamano hayo yametokana na baadhi ya wanafunzi waliohitimu ngazi ya cheti ya ufamasia kudai leseni na kuambiwa chuo hakitambuliki ndipo chanzo kiliazia hapo.

Mbogho amesema kuwa hatua mbalimbali zilishapita na kujiridhisha kuwa kinatambulika lakini wanafunzi wakitivo hicho wameendelea kuweka malumbano.

Afisa uhusiano wa chuo hicho ,Keneth Uki amesema kuwa mgogoro huo ulishapewa suluhu kwa kupitia hatua za mamlaka za serikali na kudhibitisha kutambuliwa chuo hicho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)