Pages

Kampuni ya PAN AFRICAN ENERGY yakabidhi jengo la wauguzi katika zahanati ya Nangurukuru Wilaya ya Kilwa

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega akiishukuru Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy kwa kuamua kuleta misaada kwa jamii ambayo ni ya msingi hasa Hospitali pamoja na jengo la Wauguzi lililokabidhiwa katika kijiji cha Nangurukuru wilaya Kilwa
Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy, Andrew Kashangaki (mwenye fulana nyekundu) akimkabidhi mfano wa funguo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega(wa pili kushoto) la jengo la Wauguzi la Zahanati ya Nangurukuru wilayani Kilwa. Wa kanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Peter Malekela, wapili kushoto ni Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleman Ally Bungara 'Bwege' na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa Mzee Ally Mtopa.
Meneja Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy, Andrew Kashangaki akizungumza jambo wakati wa kukabidhi jengo la Wauguzi katika kituo cha Afya cha Nangurukuru wilayani Kilwa
Mwenyekiti wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy nchini Tanzania, Patrick Rutabanzibwa akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi(hawapo pichani) kwa kuamua kutoa misaada mabalimbali katika jamii  hususani mradi huu wa nyumba za Wauguzi zilizojengwa na nguvu ya wananchi pamoja na msaana mkubwa wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy katika maendeleo ya jamii.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa Mzee Ally Mtopa akizungumza jambo
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy wakifuatilia jambo wakati wa kukabidhi jengo la Wauguzi
Jengo lililokabidhiwa na Kampuni ya Pan African Tanzania kwa ajili ya wauguzi wa zahanati ya Nangurukuru iliyopo wilaya ya Kilwa.
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy nchini Tanzania, Patrick Rutabanzibwa (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi funguo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega hii ni kuonesha ishara ya kukabidhiwa kwa jengo hilo la wauguzi

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega akipata maelezo baada ya kukabidhiwa nyumba ya Wauguzi iliyojengwa na Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy nchini Tanzania
Kikundi cha nyimbo za asili kikitoa burudani
Wakazi wa kijiji cha Nangurukuru nao hawakuwa nyuma wakati wa kukabidhiwa jengo la wauguzi
Waandishi wa habari wakiwa kazini.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)