Pages

IS yarejea kwa kishindo Kobane

IS yarejea kwa kishindo Kobane
Ripoti kutoka Syria zasema kuwa wapiganaji wa Islamic State wamerejea katika mji wa Kobane.
Wapiganaji hao wamerejea kwa mara ya kwanza tangu washambuliwe na muungano wa wapiganaji wakurdi .
Tayari watu kadha wameripotiwa kufariki katika mpaka baina ya Uturuki na Syria.
Jaribio lla kuteka miji ya Kobane na Hassakeh ni ilani kwa ulimwengu kuwa huenda wapiganaji hao wamepata nguvu mpya.
Kundili la wachunguzi wa Human Rights limesema vita hivyo vilianza baada ya bomu lililokuwa limetegwa kwa gari kulipuka katika eneo la kuvukia.
null
Mji huo wa Kobane uliharibiwa pakubwa baada ya vita vilivyoongozwa na Wakurdi kwa muungano na Marekani
Wapiganaji wa Kikurdi wanaoungwa mkono na jeshi la Marekani linaloongoza mashambulizi ya angani walikuwa wameteka mji huo wa Kobane katika tukio lililoonyesha ushindi mkubwa dhidi ya IS.
Kuna taarifa kuwa wapiganaji wa Islamic State waliingia mji wa kaskazini Hasake na kuteka maeneo mawili yaliokuwa yakithibitiwa na serikali.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)