Pages

HOSPITALI ZA APOLLO ZATOA WITO KWA WATU BINAFSI KUCHANGIA DAMU NA KUOKOA MAISHA


Ikisherehekewa kila mwaka tarehe 14 Juni Siku ya kimataifa ya uchangiaji damu inahusika katika kuinua uelewa wa umuhimu wa kila mmoja kuwa mstari wa mbele kuokoa maisha na pia kutoa shukrani kwa wachangiaji damu wote duniani. Katika nchi zinazo kua kama Tanzania upatikanaji wa damu salama ni bidhaa adimu na hasa inachangiwa na ushiriki mdogo wa raia.
Hata hivyo pamoja na shughuli zote zinazofanyika katika siku hiyo ni muhimu sana kila mmoja kutambua umuhimu wa kuchangia damu kwa hiyari. Hospitali inayoongoza kimataifa ya Apollo ni moja kati ya taasisi zilizotumia fursa hii kutoa wito kwa watanzania kuwa na utamaduni wa kuchangiaji damu sababu ya umuhimu wake katika matibabu. Mwanzilishi na mwenyekiti wa hospitali za Apollo Dkt Prathap C Reddy anasema “kutoa damu ni rahisi na kunaokoa maisha, upatikanaji wa mfumo wa kuongezewa damu nchini unatoa nafasi ya uhai kwa watu bila kujali jinsia au umri”.
Kwa wastani inakadiriwa kuwa duniani kote damu milioni 92 zinatolewa ingawa upatikanaji wa damu salama unahitajika zaidi hasa kwenye nchi kama Tanzania. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa shirika la taifa la uchangiaji damu (NBTS) mahitaji ya damu salama Tanzania ni karibu chupa 400,000 hadi 450,000 za mililita 450. uchache wa wachangiaji unamaanisha kuwa mahitaji kitaifa hayajafikiwa, katika robo ya mwaka 2015 pekee chupa 18,000 zilikusanywa. Katika nchi ambayo taasisi kubwa za afya kama Muhimbili zinahitaji chupa zaidi ya 50 kila siku namba hiyo inaonesha hatari kubwa sana. 
Kwa kuwa kuchangia damu ni tendo la hiyari Dkt Reddy anatoa wito kwa raia kuona umuhimu ambao tabia ya uchangiaji damu inaleta kwa wananchi wenzao. Tofauti na madawa na vifaa vingine vya matibabu damu haiwezi kuzalishwa kiwandani na chanzo pekee ni uchangiaji. Mtu anayefanikiwa kuishi maisha marefu kiasi kuna wakati katika maisha yake atahitaji damu au bidhaa za kuongeza damu lakini cha kushangaza ni kuwa asilimia tano tu ya watu huchangia damu mara kwa mara.
Dkt. Reddy wa hospitali za Apollo anaendelea kueleza kuwa “watu wengi hawashiriki kitendo hiki cha ukarimu hasa kwa sababu ya taarifa potofu ikiwemo kutokuelewa hatua za uchangiaji”, Sababu kubwa hasa ikiwa uoga wa kupata maambukizi wakati wa mchakato wa utoaji damu. Utimiaji wa mifuko inayoteketezwa kwa kuhifadhia damu na sindano salama kabisa unahakikisha kuwa watu hawawezi kupata maradhi ya kuambukiza kama VVU katika mchakato wa uchangiaji damu. kufuatia uchunguzi wa kimaabara uliofanyika kuangalia dalili za Hepatitis (B&C), Malaria, VVU/Ukimwi, magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na kutambua makundi ya damu ndipo damu inatumika kwenye matibabu.
Damu iliyotolewa ina matumizi mengi katika matibabu, baada ya utoaji na hatua za uchunguzi damu inatengwa katika vipengele vyake tofauti tofauti. Seli nyekundu za damu zinatumika kuongezea damu iliyopotea kwa majeruhi na wagonjwa waliofanyiwa upasuaji. Plazma mbichi iliyoganda ambayo ni sehemu ya majimaji ya damu inatumika hasa kwa wagonjwa wenye matatizo ya Ini, majeraha ya kuungua na na kesi za aina hiyo. Chembe za kugandisha damu ambazo husababisha kuganda kwa damu wakati mtu anapojikata au anapopata jeraha la wazi, hii huwa inatumika kwa wagonjwa wa lukemia na upandikizaji viungo.

Uchangiaji damu wa hiyari ni wa muhimu sana katika matibabu, ni kitendo kisicho cha kichoyo na upekee wake ni kuwa ni mchangiaji anayeunda mhimili wa benki za damu  na hivyo kuweka msingi salama na wa kuaminika katika mfumo wa uongezewaji damu nchini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)