Pages

Heri ya Kuzaliwa mwanakijiji Josephat Lukaza..Grattis på födelsedagen Josephat Lukaza

Mwanakijiji Josephat Lukaza

Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa kuweza kunifikisha siku ya leo ikiwa ni kumbukumbu ya siku yangu niliyoletwa duniani. 

Vilevile napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wazazi wangu pia kwa kuweza kunilea na kunipatia malezi yaliyo bora kwa kadri ya uwezo wao na kuhakikisha na kuwa mimi Josephat Lukaza.  

Vilevile napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru dada zangu, kaka zangu, wajomba, mashangazi na wengine wote ambao wamekuwa sehemu ya maisha yangu tokea siku ya kwanza naletwa duniani mpaka siku hii ya leo naadhimisha miaka kadhaa ya kuzaliwa kwangu.  Hata niseme niwalipe sitaweza kufika hata nusu ya kile mlichokitoa hadi kuhakikisha leo hii nimekuwa hivi bali Mungu mwenyezi ndie atakayewalipa.   

Napenda kuwashukuru wote ambao wamekuwa na mimi kama familia katika kila nyanja iwe ofisini, shule, mitaani na hata wale ambao kwa njia moja au nyingine tumeweza kufahamiana iwe moja kwa moja au kupitia watu wengine. Nasema asante sana Na Mungu awabariki sana  Heri ya Kumbukumbu ya Siku yako ya Kuzaliwa Kwa Kiswedish tunasema "Grattis på födelsedagen Josephat Lukaza"

1 comment:

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)