Pages

BELLA KUTAMBULISHA USIKU WA NASHINDWA DAR LIVE


Mfalme wa Masauti Bongo, Christian Bella ‘Obama’ akiwa ndani ya Global TV Online.
Christian Bella akiimba wimbo wake mpya wa 'Nashindwa' ndani ya studio za Global TV Online leo.
Malaika Band chini ya uongozi wa Christian Bella katika moja ya shoo yao, Dar Live patakuwa hapatoshi Jumamosi hii.
Mfalme wa Masauti akiimba.
Christian Bella akiimba kwa hisia.
MFALME wa Masauti asiye na mpinzani Bongo, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuutambulisha Usiku wa Nashindwa, Juni 6, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Akizungumza na mtandao huu, Bella ambaye ni kiongozi wa Bendi ya Malaika Music alisema kuwa kuanzia saa mbili usiku wa Jumamosi utakuwa wa aina yake kutokana na walivyojiandaa na bendi yake.
Staili mpya
Bella aliwataka mashabiki wengi kujitokeza kwa wingi kwani mbali na kuzindua wimbo huo, mashabiki watapata burudani ya kuoneshwa staili zao mpya.
“Bella na Malaika tumewaandalia staili tatu mpya na za kitofauti ambazo kila mmoja atazipenda na kuzicheza kwani tutazizindua kwa mara ya kwanza,” alisema Bella.
Sapraiz kumiminika
Bella aliongeza kuwa yeye pamoja na Malaika Music wameaandalia sapraiz kibao kwa wakazi wote wa Mbagala, Temeke na pande zote jijini Dar watakaojitokeza.
“Mara ya mwisho kupiga shoo Dar Live ilikuwa ni Usiku wa Wapendanao ‘Valentine’s Day’ na usiku ule ulikuwa maalum kwa kina mama wote nakumbuka niliwaita mashabiki wote jukwaani na kuimba nao Wimbo wa Nani Kama Mama, walifurahi sana.
“Niwaambie safari hii ni ya kitofauti kwani nakuja na Nashindwa hivyo mashabiki wote kila mmoja nitapanda naye jukwaani na kuimba naye Wimbo wa Nashindwa.”
Ladha ndani ya ladha
Ukiachana na wimbo wa Nashindwa usiku huo Bella alisema utakuwa wa ladha ndani ya ladha kwani kwa mara ya kwanza atawaonjesha wimbo mwingine mpya.
“Kuna wimbo mpya ambao nimefanya na msanii mkubwa wa kimataifa na siku hiyo mbali ya kuburudika na Wimbo wa Nashindwa pia nitawaonjesha kipande cha wimbo huo.”
Burudani mwanzo mwisho
Kuhakikisha burudani haikauki, kwa wale mashabiki 500 wataofika wa kwanza ndani ya Dar Live watapata bahati ya kupiga picha ‘red carpet’ na Bella sambamba na kuzungumza naye machache.
“Hakuna msanii ambaye amewahi kufanya hivi kama nilivyofanya Valentine’s Day na safari hii natoa nafasi hii kwa mashabiki wote watakaofika mapema.”
Mashabiki pia watarajie kupata nyimbo mpya kutoka kwa Malaika Music pamoja na nyimbo nyingine zote kali kutoka kwa Bella kama vile Nani Kama Mama, Msaliti, Nakuhitaji na nyingine nyingi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)