Pages

Wafanyabiashara walemavu wafunga barabara kwa sita eneo la makutano ya barabara ya karume na ilala

 Wafanyabiashara walemavu wakiwa wamekaa katikati ya makutano ya barabara za Uhuru na Kawawa na kufunga barabara hiyo wakipinga kubomolewa vibanda vyao na Halmshauri ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam leo mchana. Halmshauri hiyo ilivunja vibanda hivyo kupisha upanuzi wa barabara.
 Wananchi wakiwa eneo la tukio wakiwangalia wafanyabiashara hao walemavu walivyofunga barabara hizo.
Maofisa wa Jeshi la Polisi wakifika eneo la tukio kupata suluhisho.
 Wafanyabiashara hao wakiwa wamekaa mbele ya malori wakizuia yasipite mpaka kieleweke.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akiwaeleza wafanyabiashara hao maafikiano yaliyofikiwa na viongozi wao.
 Mmoja wa Wafanyabiashara hao akizungumza kwa hisia kali katika tukio hilo.
Baadhi ya utingo na vijana wakiwa wamekaa juu ya magari yao wakati wa sakata hilo.  (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)