Pages

Wadau wa mwambao kukutana kila jumapili

11231914_1144808635544922_2269725808570836614_o

Wadau wa mwambao kukutana kila jumapili kwenye kiotaa hicho kipya

Na Mwandishi Wetu
Ule usiku wa Old is Gold Taarab na Bendi yenye ubora katika muziki wa mwambao ya GUSA GUSA Min Band, Jumapili hii ya Mei 17 na Jumapili nyingine kila wiki watatoa burudani ya nguvu na ya aina yake kwenye ‘kiota’ kipya ndani ya Hugo House, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Shoo hiyo inatarajia kuanza kuanzia majira ya saa mbili usiku na kuendelea, ni ya aina yake kwa wadau na wapenzi wa taarab nchini huku kiingilio kikiwa sh 5,000 tu kwa mlangoni.

Kwa mujibu wa waandaji wa usiku huo, Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alieleza kuwa bendi ya Gusa Gusa kwa sasa hipo juu baada ya kurejea kutoka katika ziara ya nchini Uingereza waliopiga kwenye miji kadhaa na sasa wamerejea nyumbani kwa makali zaidi.
“Wadau wa usiku wa Old Is Gold karibuni sana ukumbi wa Hugo House ulipo Kinondoni, mkabala na TX Market. GUSA GUSA Min Band imejipanga kila idara uje uishuhudie” alieleza Asia Idarous.

Asia Idarous amewasihi wapenzi na wadau kujitokeza kwa wingi kushuhudia bendi hiyo pamoja na kukumbushana yale ya zamani na kubadilishana mawazo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)