Pages

Upasuaji wenye madhara madogo, hatua mpya kwa matibabu ya magonjwa ya mishipa ya moyo



Kwa kuwa magonjwa ya mishipa ya moyo ayajitokezi ghafla, inaweza kuchelewa kugundulika mpaka mtu anapopata mshtuko wa moyo. Ingawa kulingana na madaktari bado watu wengi wanaweza kujizuia na pia kutibiwa magonjwa ya mishipa ya moyo na wanashauri waanze kwa kubadili mtindo wa maisha kiafya.

Matibabu ya mishipa ya moyo (CAD) yanategemea ni kiasi gani ugonjwa umekuwa. Kubadili mtindo wa maisha ni hatua za kwanza zinazoshauriwa kwa yeyote mwenye ‘CAD’. Kiafya tabia huweza kupunguza au kusimamisha kasi ya ugonjwa na kuimarisha ubora na urefu wa maisha ya mgonjwa. Tabia hizi ni pamoja na; kuacha kuvuta sigara na kujikinga moshi wa sigara ya mvutaji mwingine, kula chakula bora, mazoezi ya mara kwa mara, kudhibiti uzito, kutuza afya ya ubongo na kudhibiti hali kama shinikizo la damu, kolesteroli na kisukari.

Kwa watu ambao ugonjwa huu umeshakuwa ndani yao, maendeleo yameleta mapinduzi katika matibabu ya magonjwa ya mishipa ya moyo. Kati ya waanzilishi ni Dkt. Sathyaki Nambala, mshauri mwandamizi na Mkuu wa kitengo cha upasuaji moyo, Hospitali ya Apollo; Bangalore. Dkt. Nambala anafahahamika kama moja ya watu wanaoongoza nchini India kwa upasuaji wa moyo, mapafu na mishipa. Anachukuliwa kama muanzilishi wa upasuaji moyo wenye madhara madogo, hatua ambayo ni bora zaidi katika matibabu ya magojwa ya mishipa ya moyo. Ni mbinu mpya na ya kisasa zaidi ya kuilinda mishipa ya moyo na magonjwa. Kama jina linavyojieleza ni vitu vichache sana vinavyotumika katika upasuaji wa moyo, katika mbinu hii moyo unafikiwa kupitia upande wa kushoto wa kifua kwa kuingia ndani kwa sentimita 4. Upasuaji unafanyika chini kidogo ya chuchu. Kifua kinapasuliwa katika mbavu pasipo kukata mfupa wowote na kwa kutenganisha nyama. Kama ilivyo kwa upasuaji wa kawaida wa moyo upasuaji huu unafanyika kwa kutumia mishipa yote au mchanganyiko wa mishipa na mishipa inayotolewa kwenye mguu. Mishipa kutoka kwenye miguu katika upasuaji huu pia huondolewa ndani kwa ndani bila kukata ngozi ya mguu. Vifaa vya kisasa zaidi na mbinu za kisasa vinaruhusu upasuaji kufanyika kwa usalama zaidi.

Kulingana na Dkt. Nyambala upasuaji wa mishipa ya moyo wenye madhara madogo una faida kadhaa kuliko mbinu za kawaida. Kwanza kabisa ni kuwa hakuna mfupa unaokatwa. Hii ina faida kadhaa katika kupunguza maumivu, mwili kufanya kazi kama kawaida, na kupumua vizuri. Tofauti na upasuaji wa kawaida wa moyo ni spidi ya kurudi kwenye maisha ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuendesha au shughuli nyingine ndogo ndogo ambazo mtu anaweza kuendelea mara baada tu ya upasuaji.

Pili, upotevu wa damu ni mdogo na pengine usiwepo kabisa jambu linalo ondoa mtu kuongezewa damu na kuepusha maambukizi katika damu na mifupa. Tatu maambukizi yote yanapunguzwa, iwe maambukizi katika kidonda au maambukizi katika mapafu baada ya upasuaji. Hii inafanya mbinu hii kuwa muhimu kwa wagonjwa wenye kisukari na wazee ambao wana kinga dhaifu kuzuia maambukizi

Nne, upasuaji huu ni wa kistaarabu na kwa kipimo cha inchi 2 hadi 3 tu kiuhalisia ni ngumu kuona kuwa upasuaji wa moyo umefanyika. Madaktari wakiwemo wale wa moyo wanaelezea inavyoshangaza kwa jinsi ambavyo upasuaji wa moyo umefanyika kupitia uwazi mdogo hivi.

“Katika upasuaji wa mishipa ya moyo wenye madhara madogo (Minimal Invasive Cardiac Surgery) hakuna kuchimba au kukata mfupa katika kifua. Mbinu ya kupitia kifua cha kushoto inaruhusu kupona haraka bila usumbufu wa kidonda”. Anasema Dkt. Nyambala anaelezea zaidi kuwa “Hatua hii ni muhimu kwa wagonjwa wa kisukari na wazee. Kiwango cha maambukizi kinakaribia sifuri na maambukizi katika mifupa yanazuilika kabisa. Mishipa yote ya moyo na kuta zake huweza kutibiwa kwa usalama, kuifanya upasuaji huu uliyo kamili usiolinganishwa na mbinu yoyote ya zamani.

Manufaa haya yote kwa pamoja yanafanya mgonjwa kuchukua muda mfupi hospitalini na kupona. Kizuri zaidi ni kuwa tofauti na mbinu za zamani, kuta zote bila kujali zilipo katika moyo huweza kupitiwa katika hali salama na ya kueleweka.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)