Kufuatia
kukua kwa teknolojia ya kompyuta kwa sasa sekta tofauti tofauti zimeweza
kuchukua fursa hiyo na kuitumia ipasavyo katika maeneo ya msingi; sekta ya
upakaji rangi pengine ni moja kati ya ambazo mtu hawezi kuzihusisha moja kwa
moja na maendeleo hayo ila hata hivyo imeweza kuendana na mabadiliko na
kuitumia teknolojia katika hatua tofauti tofauti kuanzia viwandani mpaka maeneo
ya masoko. Manufaa ya teknolojia hayawafaidishi tu wazalishaji ila pia wadau wa
biashara, mawakala na mwisho kabisa mtumiaji.
Matumizi ya
teknolojia ya kompyuta katika maeneo ya kuuzia yamefanya mapinduzi katika namna
ambazo watu wananunua vitu, shughuli iliyokuwa inafanyika muda mrefu kwa
kutumia wafanyakazi sasa zinamalizika ndani ya dakika chache. Miongoni mwa
mabadiliko ya kiteknolojia ambayo yamekuwa muhimu katika kujenga hali hii ni
mfumo wa uchanganyaji rangi unaotumika na wadau ujulikanao kimataifa kama DTS.
Mfumo otomatiki wa kuchanganya
rangi unatumia mchanganyiko wa vichupa vya rangi, kichanganyio na kompyuta
mpakato maarufu kama ‘Laptop’ ambavyo vinaunda mfumo huu wa DTS. Ikiwa moja
kati ya juhudi za kundeleza sekta ya rangi, kampuni inayoongoza kwenye
uzalishaji wa rangi nchini Insignia (Coral Paints) wamekuwa vinara katika
kuitambulisha teknolojia hii nchini. Miaka 8 iliyopita kampuni hii ilikuwa ya
kwanza kuleta wazo la kuitumia sokoni na kwa miaka mingi imekuwa na mikakati ya
kuhakikisha kuwa manufaa yanawafikia wote kwa kuwawekea technolojia hii wadau
wake na wasambazaji nchini.
Vifaa hivyo vinawekwa
katika maeneo ya wasambazaji na zina ruhusu mabadiliko yoyote ya uzalishaji wa
rangi kulingana na anavyotaka mteja. Kwa wasambazaji mbinu hii inaleta faida
mbalimbali kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupunguza mzigo kwani msambazaji
hatahitaji kuwa na mzigo mkubwa. Badala ya kuhifadhi rangi nyingi tofauti
tofauti, msambazaji anahitaji kuhifadhi rangi kuu na tona na kwa kutumia
mashine hiyo ana kua na uwezo wa kutengeneza rangi yoyote katika kadi hapo hapo.
Mashine hii inachanganya kwa kutumia rangi za msingi. Ni mali muhimu ki
biashara kwa muuzaji ambayo inarahishisha uendeshaji na kumawasaidia kuepuka
kuishiwa na akiba au kukaa na bidhaa zisizo na muhimu.
Tangu kutambulishwa kwake DTS
imekuwa chaguo la msingi kwa wadau wengi katika sekta ya rangi. Bw. Kishan Dhebar, Mkurugenzi Mtendaji wa
Coral Paints, anaelezea kwamba “DTS
ina faida kadhaa na imekuwa mshirika wa karibu katika kukuza maendeleo ya sekta
ya rangi. Mzigo mdogo na matokeo ya haraka inasaidia kuridhisha wateja ambapo
pia inaongeza mafanikio kwa mfanya biashara” Bw. Kishan pia akiongelea manufaa ambayo mtumiaji wa mwisho anapata
kwa kutumia teknolojia hii wakati wa kununua anasema “gharama ya kuchanganya rangi katika mashine ni ndogo kuliko kununua
rangi hiyo ikiwa imesha changanywa kutoka kiwandani kutokana na bei ndogo ya
rangi za msingi. Bidhaa nyingi zinaweza kutumika katika mashine kuzalisha rangi
mbalimbali. Hivyo wateja hawafaidiki tu kwa gharama kuwa nafuu lakini pia
wanaokoa muda sababu ya huduma ya papo
kwa hapo na uhakika wa upatikanaji wa zaidi ya michanganyiko 10,000”
Wakiwa wamekamata sehemu kubwa ya soko
la rangi na sekta ya upakaji rangi na wakiendelea kusukuma nia ya ugunduzi
katika nyanja tofauti tofauti Coral Paints wanaendelea kushikilia nafasi yao ya
uongozi kwenye sekta ya rangi Tanzania siyo tu kwa wingi/ujazo na thamani
lakini pia kupitia kutambulisha na kutumia teknolojia mpya pamoja na kuongoza
hatua ambazo zimekuwa zikifungua njia.
Kuhusu
Insignia
Mwaka 1989, Tanzania ilishuhudia kuzaliwa Coral
Paints, kampuni ndogo ambayo ingeweza kubadilisha uso wa sekta ya rangi nchini.
Ikiendeshwa na dhamira ya kipekee na ubora, kampuni ambayo kwa sasa inajulikana
kama Insignia Limited, ilikua kwa kiwango kikubwa na kuvuka mipaka.
Hivi leo, Insignia imefikia moja ya malengo yake;
ni moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa
rangi mbalimbali. Uamuzi wake wa kuleta bidhaa zenye viwango vya hali ya juu
nchini Tanzania umewezeshwa na ushirikiano na makampuni makubwa ya kimataifa
kama Marmoran (Pty) Ltd, iliyopo Africa ya kusini, Ronseal iliyopo nchini Uingereza na Pat’s Deco ya Ufaransa.
Bidhaa mbili za Coral na Galaxy, zinafafanua ubora wa
kampuni ya Insignia. Chini ya majina haya, kampuni inatengeneza rangi na bidhaa nyingine nyingi. Teknolojia ya hali ya juu
ipatikanayo katika kampuni hiyo inaipatia kampuni hiyo msaada mkubwa sana katika ushindani. Rangi ya Galaxy
inatngenezwa kiufundi, inatumia ujuzi, pembejeo na washauri wa kimataifa, inawapatia wateja wake
teknolojia ya kisasa kwenye rangi. Rangi ya Coral paint ni bidhaa inayoongoza katika soko nchini
Tanzania. Imepata kibali, na kuimarisha sifa yake kama bidhaa yenye ubora
inayoedana na thamani- ya -fedha.
Kiufanisi, miundombinu ya Insignia inajulikana kwa ubora
wake. Viwanda vyake vina vifaa vyenye ubora na vya kisasa
vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya kimataifa.
Kampuni hii ina viwanda jijini Dar es Salaam,
Moshi, Mwanza na Zambia pia ina Vituo vya usambazaji mkoani Moshi, Arusha,
Mbeya na Mwanza mikoa mikubwa nchini.
Pia kuna uwepo wa mtandao mpana wa wafanyabiashara na malori ya kisasa kuwahakikishia
usambazaji wa bidhaa nchini kote. Kampuni hiyo pia ina vituo nchini Rwanda, Burundi
na Malawi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)