Pages

Swali la Msingi Kutoka Kwenye Daladala leo: Je ni lazima kondakta kutaja vituo kwa abiria wake?

Jana wakati nimepanda daladala nikitokea home kuelekea kibaruani wakati daladala hiyo imefika Ubungo darajani basi hilo lilikua likielekea Makumbusho basi kondakta kama kawaida yao wakatangaza vituo wakati anatangaza kituo kinachofuata wadau waliokuwa wanashuka katika kituo hiko cha mbele ya supa staa wakaanza kusogea kwaajili ya kushuka basi lilipofika kituoni hapo likasimama na abiria wakashuka mara baada ya kushuka basi likaendelea na safari yake huku kondakta akatanza kituo kingine kumbe wakati anatangaza mmoja kati ya abiria alikua anashuka katika kituo hiko cha Kivulini, Kondakta yule alitangaza kituo hiko kabla hajafika kituo hapo na muhusika akusikia baadae basi lishavuka kituo hiko ndipo muhusika akamwambia Kondakta kuwa amshushe kivulini huku wakati huo gari limeshakolea mwendo gari likaendelea na safari na kwenda kusimama kituo cha Mlimani City.

Mara baada ya basi kusimama katika Kituo Hiko cha Mlimani City Abiria walioshuka katika kituo hiko wakashuka na yule abiria aliyetakiwa kushuka kituo cha nyuma ya mlimani city ambacho ni kivulini nae akashuka aliposhuka akagoma kulipa nauli kisa amepitishwa kituo basi ukatokea mzozo kati ya kondakta na abiria huyo, mzozo ukawa mzozo ndipo dereva naye akashuka kuangalia tatizo nini si ndio hapo sasa abiria yule akaeleza kuwa wamempitisha kituo akaulizwa wakati kondakta anatangaza ulikua wapi?Na je ulisema unashuka wapi kwahiyo we tupe nauli yetu abiria akaamuliwa hivyo kama ilivyo kawaida mtu akihisi kaonewa huwa anatafuta huruma kwa abiria wenzie si ndio hapo akawa anawaambai dereva na konda wake mimi nilisema mnishushe mapema kabla gari halijapita na ukitaka kuamini muulize huyo mama hapo akamuonyeshea yule mama, Konda na dereva wake bila hiyana wakamuuliza huyo mama unajua alijibu nini huyo mama Akamwambia Abiria yule kuwa alichelewa kumwambia konda anaposhuka na alisema wakati gari lishapita kituoni 

Basi mziki ukawa hapo ndipo abiria walipoanza kumuwakia yule abiria mwingine wengine wakisema si utembee tu ni hapo wengine wakasema fanya mazoezi siku moja moja tu na wengine wakaendelea kukaa kimya huku mimi binafsi nikijiuliza maswali mengi huku swali moja tu na la msingi ambalo nilijiuliza Hivi Ni lazima Kondakta ataje vituo? Na Je wewe abiria kwani Hujui uendapo mpaka Usubiri kutajiwa kituo na abiria? Na kama hupaji kuna ubaya ukiuliza? hayo ndio maswali ya msingi sana niliyojiuliza nikasema isiwe shida ngoja niulize wasomaji wangu leo Je ni lazima Kondakta kutaja vituo ambavyo abiria wake wanashuka?

Hili ndio swali letu la msingi kwa leo...Tupe majibu yako hapa chini sehemu ya coment na sisi tutayatoa hewani hapahapa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)