Pages

STEPHEN WASSIRA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS

Stephen Wassira akitangaza nia ya kuwania Urais kwenye Ukumbi wa wa BOT jijini Mwanza leo.
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira leo ametangaza nia ya kuwania Urais kwenye Ukumbi wa wa BOT jijini Mwanza.
Wassira anawania nafasi ya kugombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika hotuba yake wakati wa kutangaza nia yake, Wassira amesema amepata kuteuliwa kuongoza sehemu mbalimbali nchini maana marais wote wa awamu nne walikuwa na imani naye.
Pia amewashukuru wageni waalikwa waliofika kwenye ukumbi kutoka sehemu mbalimbali kwa kuweza kufika na kumuunga mkono huku wakiwa na imani naye.
Kauli mbiu yake ni katika mbio hizo ni Uchumi Imara kwa Tanzania mpya.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)