Pages

Stendi kuu mjini Iringa waanzisha timu ya mpira wa miguu ya KIBIKI FC

Kibiki azizungumza na kijana, fundi viatu wa mjini Iringa!

 


Na mwandishi wetu, Iringa
 

VIJANA wa stendi kuu ya mabasi ya mjini Iringa, wameanzisha timu ya mpira wa miguu ya ‘Kibiki Football Club’ili kuunga mkono harakati za mwanahabari wa gazeti la Uhuru na mzalendo, baada ya kutangaza nia kuwania jimbo hilo.
  


Katibu wa timu hiyo, Charles Manet alisema wameamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu inayoitwa Kibiki, ili kuonyesha dhamira yao ya dhati katika kumsaidia kijana mwenzao.
 
“Yeye mwenyewe hakujua kama tumetumia jina lake kwenye timu yetu, tayari tumeshacheza mechi mbili tangu timu yetu ianze kuitwa Kibiki FC na tunatarajia kuendelea kucheza mechi za kirafiki, tukianza na timu ya Wambi ya stendi kuu ya mjini Mafinga,”alisema
 
Maneti alisema wamekuwa wakisafiri kwa kuchangishana fedha na kwamba tayari wamepata jezi seti moja, kutoka kwa wadau mbali mbali wa michezo mjini Iringa.
 
Aliwataka wapenzi wa soka la mjini Iringa kuunga mkono jitihada za vijana hao katika kuhakikisha, timu hiyo inasonga mbele badala ya kuikatisha tama.
 
“Pamoja na kukatishwa tama tangu tuunde timu hii lakini ukweli ni kwamba, hatutaacha kwa sababu Kibiki ni kiongozi na tusipomuunga mkono kijana mwenzetu tutakuwa hatujamtendea haki hata kidogo,”alifafanua.
 
Kabla ya kuunda timu hiyo vijana hao, walichangishana fedha zaidi y ash laki moja na kumkabidhi Kibiki, wakimtaka azitunze kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Iringa, muda ukifika.
 
Wakizungumzia ubunge, vijana hao walisema kuwa jamii ya wana Iringa inatarajia kumpata kiongozi anayetokana na wenyewe, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ili wampigie kura ya kuwa mbunge wa jimbo hilo na sio vinginevyo.
 

Tangu alipotangaza nia ya kuwania jimbo hilo, Kibiki amekuwa akikubaliwa na makundi mbalimbali wakiwemo vijana, walemavu, wanawake na wazee.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)