Pages

PPF yapata cheti cha ubora wa kimataifa ISO 9001:2008

 Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF, Ndg William Erio (katikati) akiwa ameshika cheti cha kuthibititshwa kwa Ubora wa huduma zao na Shirika la Viwango la Kimataifa la ISO na kupatiwa cheti namba ISO 9001:2008. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa PPF, Ndg Julius Kam Mganga na kulia ni Mkurugenzi wa Majanga wa PPF, Uphoo Swai.
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa PPF, Ndg William Erio (katikati) akifafanua juu ya hatua zilizofuatwa na Shirika la Viwango vya Kimataifa na kufikia hatua ya kuitambua PPF kwa utoaji bora wa huduma kwa ngazi ya kimataifa.

  Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya PPF mtaa wa Samora
 Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali wakifuatilia mada kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa PPF wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya PPF mtaa wa Samora
Mkurugenzi Mkuu wa mfupo wa pensheni wa PPF,  Ndg Emmanuel Urio akijibu moja ya maswali aliyokuwa akiulizwa na waandishi wa habari (hawapo Pichani) wakati wa kutangaza na kuonyesha cheti walichopatiwa na shirika la Viwango la Kimataifa la ISO na kupatiwa cheti namba ISO 9001:2008.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa PPF, Ndg William Erio leo ameitambulisha PPF kuwa ndio mfuko wa kwanza wa hifadhi za jamii Nchini kwa kutambuliwa Kimataifa na shirika la viwango la kimataifa ISO kutokana na ubora wa huduma zake na kukabidhi hati na shirika hilo la Viwango la Kimataifa lenye Makao Makuu yake Nchini Uingereza.

Akiongea na wanahabari mapema leo, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Ndg Erio ameonyesha hati ya Kutambuliwa na Shirika la Viwango la Kimataifa ambapo amesema kuwa Shirika hilo limeitambua PPF kuwa ndio shirika linalotoa huduma zenye viwango vya kimataifa na kupelekea Kutambuliwa na Shirika hilo la kimataifa na hatimaye kukabidhi hati yenye namba ISO 9001:2008.

1 comment:

  1. Anonymous11:16 AM

    Sio kwamba ppf ndio wa kwanza kupata,nssf pia wana cheti cha ISO

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)