Pages

News Alert: Sepp Blatter ashinda tena kuiongoza Fifa kama rais

Aliyekuwa rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA Sepp Blater ambae alikuwa mmoja kati ya wagombea nafasi hiyo ya urais katika uchaguzi uliofanyika leo Ameshinda tena nafasi hiyo na sasa kuitumikia FIFA kwa kipindi cha miaka 18 tokea aliposhika nafasi hiyo.

Blatter aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wajumbe, katika siku ya pili ya mkutano mkuu wa shirikisho hilo la kandanda duniani huko Zurich Uswisi.
Blatter ameahidi kukamilisha mabadiliko yatakayoirejeshea FIFA hadhi yake.
Blatter anakabiliana na mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo utakaofanyika leo.
Kwa upande wake mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan anasema kuwa yeye pekee yake ndiye aliye na nia ya kuleta mabadiliko ya kimsingi yatakayomaliza ufisadi na ulaji rushwa ndani ya FIFA.
Takriban wenyeviti wa mashirika 209 ya kandanda kote duniani wanakura moja kila mmoja .
Mwaandishi wa habari wa BBC, anasema kuwa Bwana Blatter anategemea uungwajji mkubwa kutoka kwa wajumbe wa mataifa ya Amerika, Afrika na Asia - ambao wanasema kuwa amefanya mengi katika kuboresha mchezo wa kandanda katika mataifa maskini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)