Pages

Mcheza sinema maarufu nchini India Salman Khan ahukumiwa kwenda jela miaka mitano

Salman Khan mwenye miwani meusi
Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan amekuhumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtu mmoja asiye na makazi alipokuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa mjini Mumbai.
Khan alikuwa ameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kuelekeza gari lake kwenye kundi la watu waliokuwa wamelala kwenye njia kando ya barabara mwaka 2002. Mmoja kati ya watu hao Noor Ullah Khan alikufa katika ajali hiyo.
Khan amedai kuwa dereva wake ndiye anayepaswa kulaumiwa lakini mashuhuda wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa kwenye usukani na alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa jaji wa mahakama hiyo mwigizaji huyo anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)